Mwenyekiti
wa Soko la Ilala Mchikichini, Jumanne Kongogo, akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kupungua
vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya kufanyika
kampeni mbalimbali za kupinga ukatili huo zilizofanywa na Shirika la
Equality for Growth (EfG) kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mwenyekiti
wa Soko la Kisutu, Taminu Chande, akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kupungua vitendo vya
ukatili katika soko hilo. Kushoto ni Katibu wa soko hilo, Suitbert
Nyawalla.
Mfanyabiashara
wa soko la Ilala Mchikichini, Denis Ngaiza (kulia), akizungumza katika
mkutano huo. Wengine ni wafanyabiashara wa soko hilo. Kutoka kushoto ni
Yasin Kiluwa, Tatu Shehe na Samilla Kirundwa.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko la Ilala Mchikichini,
Betty Mtewele (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, kuhusu kupungua kwa vitendo vya ukati wa kijinsia katika soko hilo
baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa elimu ya kupinga
ukatili huo. Wengine ni wafanyabiashara wa soko hilo.
Mwezeshaji
wa kisheria katika soko la Ilala Mchikichini, Charles Beatus
(katikati), akizungumza. Kulia ni Mwezeshaji wa kisheria, Eva Kakobe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko la Ilala Mchikichini, Betty Mtewele.
Mwezeshaji wa kisheria, Domitila Ngwada (kulia), akichangia jambo.
Mfanyabiashara wa Soko la Kisutu, Abdallah Mkumba (kulia), akichangia jambo. Kutoka kushoto ni Juma Khalid na Jumanne Ally.
Mfanyabiashara wa Soko la Kisutu, Rose Bruno, akizungumzia kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Equality for Growth (EfG) limetajwa kusaidia kupunguza vitendo vya
ukatili wa kijinsia katika masoko ya Ilala Mchikichini na Kisutu jijini
Dar es Salaam.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wafanyabiashara, viongozi wa masoko hayo pamoja na
wasaidizi wa kisheria Dar es Salaam jana wamesema baada ya shirika hilo
kutoa mafunzo na kufanya kampeni mbalimbali za kupinga ukatili huo hali
imekuwa tofauti na awali.
"Soko
letu la Mchikichini lilikuwa na kesi nyingi za vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia kutokana na muingiliano wa watu hasa vijana
kutoka katika maeneo yasiyo rasmi waliyokuwa wakifanyia biashara na
kuhamia hapa kwetu" alisema Mwenyekiti wa soko hilo Jumanne Kongogo.
Alisema
vijana wengi walihamia katika soko hilo wakitokea Manzese, Kariakoo,
Mnazi Mmoja, Buguruni na maeneo mengine ya jiji na hata nje ya Mkoa wa
Dar es Salaam.
Alisema
baada ya EfG kufanya kampeni za kupinga ukatili huo na watuhumiwa
kupigwa faini ya sh. 50,000 vitendo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika soko hilo, Betty Mtewele
alisema mafunzo waliyopata kupitia shirika hilo yamewafanya wanawake
kujiamini na kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwezeshaji
wa kisheria katika soko hilo Charles Beatus alisema matokeo ya kazi
wanayoifanya ni makubwa mno baada ya kupata mafunzo kwa kuwezeshwa na
shirika hilo.
Alisema
kupitia kamati walioiunda wamefanikiwa kupunguza vitendo hivyo kwa
asilimia kubwa kwani kupitia kamati hizo mtu akibainika kufanya
udhalilishaji wowote amekuwa akiitwa mbele ya kamati.
Mwenyekiti
wa Soko la Kisutu Tamimu Chande alisema katika soko hilo vitendo hivyo
havipo na kama vitakuwepo basi vitakuwa vinafanyika kwa usiri bila wao
kujua.
Katibu
wa Soko hilo, Suitbert Nyawalle alisema mafunzo na kampeni zilizofanya
na EfG katika soko hilo zimeonesha mafanikio makubwa.
"Niseme
kuwa kampeni zilizofanywa na EfG zimewafanya wafanyabiashara katika
soko hilo kujielewa na kujua kumfanyia mtu kitendo cha udhalilishaji
pamoja na kumtukana ni kosa kisheria" alisema Nyawella.
Nyawella
aliongeza kuwa mwaka juzi baada ya EfG kufanya tamasha la kupinga ukati
wa kijinsia katika soko hilo kunamfanyabiashara mmoja alitenda kosa la
udhalilishaji na alipopelekewa wito wa kuitwa alitoroka na mpaka leo hii
hajarudi katika soko hilo kwa kuogopa asidakwe na mkono wa sheria.
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa shirika hilo Shabani alisema shirika lao
limekuwa likifanya kampeni ya kupinga vitendo vyote vya ukatili wa
kijinsia katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza na Tanga na kwa Dar es
Salaam wameendesha kampeni katika masoko ya Ilala Mchikichini, Temeke
Sterio, Gezaulole, Ferry, Kisutu na Tabata Muslim.
Alisema
kampeni yao ya kwanza ilikuwa ni Mpe Riziki na Si matusi na imesaidia
sana wafanyabiashara kujielewa na kutambua suala zima la unyanyasaji wa
kijinsia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269