Mtaalamu
wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo,
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Hoteli ya Lamada
jijini Dar es Salaam leo wakati akifafanua kuhusu sheria ya haki miliki
ya kazi za wasanii wa muziki.
Rais wa Tanzania Music Foundation (TMF) Dk. Donald Kassanga
akifafanua mambo kadhaa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na TMF,
kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na dawa za kulevya.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba akizungumza katika mkutano huo.
Dotto Mwaibale na Christina Mseja
WADAU wa muziki wa injili
wanatarajia kukutana kesho kutwa Machi 4 mwaka huu kwenye Kongamano la
Wasanii wa muziki huo litakalofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ustawi
wa Jamii Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk.
Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo, alisema kongamano hilo lina dhumuni
kubwa katika kujenga uelewa kwa wasanii wa muziki juu ya kazi zao,
hususani changamoto na suluhu za kazi za Sanaa.
Kyogo alisema kazi za Sanaa ni
mali na zimekosa ulinzi na hakuna jitihada zozote zinazoendelea katika
kusaidia wasanii hao.Wasanii wamekosa ubunifu na watu wamekata tamaa na
kujiingiza katika wimbi la dawa za kulevya. Kuwepo kwa mapungufu ya
adhabu haipunguzi uhalifu kwani wasimamizi wa sheria wanatakiwa kuwa na
uwezo zaidi katika sheria hizo.
“Lazima kuwe na sheria ya makosa
ya wizi za kazi za wasanii kwani itasaidia kupunguza wizi na itaongeza
kipato na ajira, kwa kuwa muziki ni mali ya jamii na ni afya na tiba”,
alisema Kyogo.
Rais wa Tanzania Music Foundation
(TMF) Dk. Donald Kissanga aliongeza kuwa lengo kubwa kongamano ni
kuhakikisha serikali inatengeneza mazingira bora katika tasnia nzima ya
muziki jambo litakalosaidia kuongeza pato la taifa.
“Watu wamekuwa wakiiba kazi za
wasanii na kama TMF tunalaaani na kuomba serikali kupitia vyombo vya
dola kuziba mianya hiyo" alisema Kissanga.
Katika hatua nyingine Kissanga
alisema TMF kinaungana na Serikali katika mapambano ya dawa za kulevya
nchini kwani waathirika ni pamoja na wanamuziki na wasanii kwa ujumla.
Mwimbaji wa nyimbo za injili,
Faraja Ntaboba, alisema kuwa wasanii wamekuwa wakiibiwa sana kazi zao
wakati wanatumia nguvu kubwa kwa kuziandaa.
"Tuna amini endapo Serikali
ikisimamia vizuri kwa kushirikiana na TMF wataweza kulipa kodi sawa
sawa na kuendesha kazi vizuri" alisema Ntaboba.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269