Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama,
akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 26 wa Wamachama na Wadau wa PPF
kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha,
(AICC), jijini humo jana Machi 24, 2017. Kauli mbiu ya Mkutano huo ilikuwa, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”.
Katika
hotuba yake pamoja na mambo mengine, Waziri alisema"Naomba niwatoe hofu
Wanachama wa PPF, kuhusu uamuzi wa Mfuko kuwekeza kwenye viwanda, kwani
uamuzi huu ni sahihi kwa sasa, ikizingatiwa ni utekelezaji wa Mpango
wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano
wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati
ifikapo
mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda, lakini pia Serikali ya
awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa
kujenga uchumi wa viwanda." Alitoa hakikisho Waziri Mhagama.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, Bw.William Erio, akionyesha furaha yake kufuatia mafanikio
makubwa yaliyofikiwa katika mkutano huo ambapo alisema, jumla ya
washiriki 800 walihudhuria mkutano huo na hivyo Mfuko umefanikiwa kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu
ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya
ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5,
(2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na
uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira
zitakazoongezeka.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Yeye alisema Jeshi la Magereza limeamua kushirikiana na taasisi
mbalimbali ikiwemo PPF na NSSF katika kutekeleza mipango ya serikali ya
kujenga uchumi wa viwanda, ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na PPF,
wanafanya uwekezaji mkubwa katika kiwanda cha viatu kule gereza la
Karanga mkoani Kilimanjaro na kwenye kiwanda cha sukari kwenye shamba la
Mbigiri mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, akifuatilia kwa makini mkutano huo
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, kilichoko mkoani
Morogoro Nicander Kileo, akitoa mada juu ya uwekezaji wa kiwanda hicho ambacho
kitamilikiwa kwa ubia baina ya Mifuko ya PPF na NSSF wakati wa mkutano wa 26 wa
Wanachama na Wadau wa PPF ambao umeingia siku ya pili naya mwisho jana Machi
24, 2017.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, kilichoko mkoani
Morogoro Nicander Kileo, akitoa mada juu ya uwekezaji wa kiwanda hicho ambacho
kitamilikiwa kwa ubia baina ya Mifuko ya PPF na NSSF wakati wa mkutano wa 26 wa
Wanachama na Wadau wa PPF ambao umeingia siku ya pili naya mwisho jana Machi
24, 2017.
Mratibu
wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkulazi huko mkoani Morogoro,
Bi.Radhia Tambwe akitoa mada kuhusu uwekezaji huo ambao unafanywa kwa ubia na
Mifuko ya PPF na NSSF.
|
Mchokoza
mada ya uwekezaji katika viwanda, Profesa Humphrey Moshi akizungumza.
|
Mkuu
wa wilaya ya Arusha, Gabriel Fabian
Daqqaro, akizungumza kwenye mkutano huo.
|
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa
kipindi ndani ya mkutano huo, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini
ya PPF, Bi.Amelye Nyembe
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, akifuatilia mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Msemwa, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiendelea
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, akifurahia jambo
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, Bw. Meshack Bandawe,
akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uwekezaji na
Mifuko hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo, (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw.Gabriel Fabian
Daqqaro.
Waziri Mhe. Jenista Mhagama
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, (PAC), Mhe.Naghenjwa Kaboyoka, akizungumza kwenye mkutano huo |
Mwenyekiti wa kikao, Mhe.Amelya Nyembe, akizungumza
Wafanyakazi
wa PPF wakipoz kwa picha wakati. Wafanyakazi hao ni sehemu ya kamati ya
maandalizi ya mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Ramadhan Khijjah, akisikilzia kwa makini watoa mada
Washiriki wakiimba wimbo wa Taifa
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitoelwa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269