Breaking News

Your Ad Spot

Mar 11, 2017

WAZIRI WA HABARI ,UTAMADUNI NA MICHEZO MH NAPE NNAUYE AONGOZA TULIA MARATHONI JIJINI MBEYA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Akiwaongoza wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye Mbio za Tulia Marathoni zilizofanyika jijini Mbeya akiwa ameambatana na aibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu Pamoja na Wadau Mbalimbali waliojitokeza kwenye Mbio hizo leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Leo ameongoza Wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwenye Mbio za Tulia Marathoni zilizoandaliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu Kupitia Taasisi yake ijulikanayo kama Tulia trust. Mbio hizo zilizohusisha KM 21 ,KM 5 na KM 2 kwa wazee zilifana baada ya Wakazi Wengi wa Mbeya Kujitokeza kwa Wingi Wakiwemo Viongozi Mbalimbali na Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao Hapa Nchini,Lengo la Mashindano hayo ni kupata fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya na elimu hususani uboreshaji Majengo na vyoo katika sekta hizo.
  Rais wa Chama cha Riadha Nchini na Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Mh Anthony MtakaAkimweleza Jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu kabla ya Mbio za Tulia Marathoni zilizofanyika Jijini Mbeya leo wakiwa Pamoja na  Pamoja naAfisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange
 Tulia Marathon lengo lake ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya na elimu, maeneo yanayolengwa kwenye afya ni Kituo cha Afya cha Ruanda kilichopo Mwanjelwa na Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana ambako utafanyika uboreshaji wa wodi ya wazazi,”

 Katika Elimu maeneo yanayokusudiwa kuboreshwa ni pamoja na Shule ya Wasichana ya Loleza ambayo itafanyiwa maboresho kwenye mabweni mawili na vyoo pamoja na shule tatu za msingi,” alisema Lwiza.Mshindi wa Mbio hizo Amejishindia kitita cha Sh. Milioni moja wa Pili Sh. 700,000 na wa tatu atapata Sh. 500,000.Katika Mbio fupi za kilomita mbili ambazo ziliwahusisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwamo Naibu Spika Mwenyewe .
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange  Waliposhiriki Mbio Hizo leo Jijini Mbeya.

 Rais wa Chama cha Riadha Nchini na Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Mh Anthony Mtaka akiwa na Afisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange pamoja na Mdau Hassan Ngoma.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages