Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na
kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua
mikononi.
Ameyasema hayo baada ya
kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya
kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na
kutelekeza kiliwili chake.
“Kwanini watu wajichukulie
hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti
huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote
na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa
tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela
Kasesela alisema kama wilaya
wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia
sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la
polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.
“Wilaya ya Iringa ilikuwa
imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye
uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na
lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina
kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela
Kasesela ameeleza kuwa tukio
hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani
nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.
Aidha Kasesela amewaomba
viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya
kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.
Kwa upande wake afisa
mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa Mnamo tarehe
06/04/2017 huko kitongoji cha Utitiri kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihorogota
tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa alisema kuwa Hassan Nyalusi
alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na mwili
ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu
wa marehehemu kwa taratibu za mazishi laiki mtu mmoja Jackson Nyalusi anashikiliwa
na polisi kuhusishwa na mauaji haya,bado upelelezi unaendelea
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269