NA OCTAVIAN KIMARIO-WHUSM DODOMA
Wazo
la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia
na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.
Akijibu
swali la Mbunge wa Mchinga Hamidu Hassan Bobali aliyetaka kujua kauli
ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa
ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza
kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani.
“Kufuatia
majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale
kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha
shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha
uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo
hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike
katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi” alisisitiza
Mhe. Makani.
Kuhusu
Serikali kupunjwa mapato yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu
Viumbe ya Berlin, Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani
ni ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi kutoka
Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia kutoka nchi
mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho hiyo hutolewa na
Serikali ya Ujerumani.
Ameeleza
kuwa Serikali ya Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na
Malikale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa
wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale nchini.
Mijusi
mikubwa (Dinosaria) ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru,mkoani Lindi kati ya
waka 1909 na mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya
Berlin nchini Ujerumani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269