Breaking News

Your Ad Spot

Jun 19, 2017

WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI WARIOBA APONGEZA MSIMAMO WA RAIS DK. MAGUFULI JUU YA ULINZI WA RASILIMALI ZA NCHI

Na Judith Mhina - MAELEZO
WAZIRI Mkuu Mtaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Joseph Sinde Warioba amempongeza Rais John Magufuli kwa kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Madini ya Barrick Prof. John Thornton juu ya namna Kampuni hiyo itakavyoweza kulipa fedha za madini ambayo yalikuwa yakisafirishwa nje ya nchi kwa njia ya udaganyifu.

Jaji Warioba ametoa pongezi hizo leo nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar Es Salaam katika mahojiano maalumu na Idara ya Habari MAELEZO kuhusuiana na hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli baada ya kupokea taarifa mbili kutoka kwa Kamati alizoziunda kuchunguza mchanga wenye madini (Makinikia) uliokuwa unasafirishwa kwenda nje ya nchi.

Amesema kwamba, mazungumzo baina ya Rais na Bwana Thornon ambaye ana hisa kubwa zaidi (64%) katika Kampuni Mama ya Acacia inayohusika na usafirishaji wa madini kwenda nje ya nchi yamerejesha imani ya Watanzania juu ya uporwaji wa rasilimali ya nchi uliokuwa unafanywa kwa miaka mingi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya pili iliyoundwa na Rais Magufuli, thamani ya Makanikia yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda njenya nchi kuanzia mwaka …ni Trilionin 108 fedha za Kitanzania.

Tuipe nafasi Serikali ifanye mazungumzo na mmiliki huyo na maamuzi yatakayofikiwa tukubaliane nayo, tumuamini Rais kwa kile anachokifanya badala ya kuanza kusema , mmiliki huyo alipe fedha yote ya trilioni 108, hivyo ni kuhukumu kabla ya mazungumzo, ambapo sio sahihi hata kidogo aliongeza Warioba.

Pia, Jaji Warioba amesema “Watanzania ni lazima tujiamini kuwa tunaweza, kwa kweli namshukuru sana Rais kwa kutufumbua macho na kuonyesha njia kuwa watanzania wanaweza kudai haki yao pale wanapoamua kuisimamia kikamilifu”.

Aidha, Jaji Warioba ameonya tabia ya baaadhi ya viongozi ya kulalamika yanapojitokeza matatizo ndani ya nchi badala ya kumsaidia Rais kutafuta ufumbuzi wake akitolea mfano wa suala hili la Makinikia ambalo wameanza kumlaumu mtu mmoja mmoja. Katika suala kama hili, kila mtu au Taasisi inatakiwa kumuunga mkono Rais na kumsaidia  katika kuhakikisha kwamba rasilimali ya nchi inalindwa na kutumika kwa manufaa ya Watanzania wote.

“Tatizo la Watanzania tunaangalia Taasisi au mtu mmoja mmoja. Nashangazwa sana na migawanyiko hii ambayo inatugawa zaidi badala ya kutufanya wamoja, tusiruhusu hili. Tusiangalie mtu binafsi, Chama au Taasisi, nadhani ni busara tukasema tumekosea kama Watanzania na sasa tutoe mawazo ya kujenga na kuboresha utendaji ambao utafanya kila Mtanzania kufaidika na rasilimali za nchi yetu.” Amesema Jaji Warioba.

“Tutambue kwamba,  mfarakano wowote hutokea katika masuala ya kitaifa kama haya ya rasilimali za nchi, hivyo tusinyosheane vidole tutafute ufumbuzi wa matatizo yetu kwa pamoja kama nchi kwa masilahi ya vizazi vya sasa na vijavyo,” alifafanua zaidi Jaji Warioba.

“Namuunga mkono Rais kwa kuwa amesema angependa kupata maoni kutoka kwa viongozi na watanzania kwa ujumla ni kwa jinsi gani tunaweza kuboresha hali ya ukusanyaji wa mapato ya madini,  mawazo gani yatasaidia kuimarisha Sera, Sheria, na taratibu kuliko kuendelea na malumbano na kushurutisha kuwaadhibu viongozi waliopita.” Alisisitiza Waziri Mkuu huyo Msaafu.

Jaji Walioba ambaye amewahi pia kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais amesema, Rais wetu ni kiongozi ambaye anahitaji kupata usaidizi wa kutosha kutoka kwetu kama Wananchi na hasa Wasaidizi wake na Serikali kwa ujumla. “Rais hawezi kufanya kazi peke yake naomba tuimarishe utendaji wetu wa kazi. Kama utendaji ungekuwa mzuri suala la Makontena kufika hadi bandarini lisingekuwepo, na hata kugundulika kwake kusingefanywa na Mheshimiwa Rais,” 

Nampongeza sana Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwanamke, Mama Samia Suluhu Hassan na  Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa utendaji wao wa kazi, ambao ni wasikivu na wanatekeleza kazi zao bila mihemko wanatoa maagizo na kufatilia kwa wahusika ili watekeleze.

Warioba alimalizia na kusema: “Mara baada ya Uhuru wa Tanganyika kila mwananchi na viongozi tulilaumu wakoloni kwa kila baya lililokuwa linatendeka au kutokea, kutokana na hilo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akasema nanukuu “ Kweli Tanganyika imefikia hapa tulipo  kutokana na wakoloni, lakini hatuna budi kukabiliana na changamoto hizi na kujenga nchi yetu”  Mwalimu aliamua kuja na Waraka wa “Act don’t Argue“ na leo hii tumeona changamoto imetolewa hivyo ni lazima kutoa maoni ili tutoke hapa tulipo sio kunyosheana vidole.

Sio kweli kwamba hali ilivyo sasa ni mbaya kuliko awamu ya kwanza au ya pili. Lakini wakati ule kilichotusaidia ni umoja wetu na mshikamano wa kutatua matatizo yetu kwa pamoja hatukuachiwa kama viongozi tufanye wenyewe. alihoji Warioba.

Warioba alisisitiza “iweje leo tumuachie Rais afanye kila kitu mwenyewe naomba sana tumsaidie na kumuunga mkono hakika ana nia njema kabisa na rasilimali za nchi hii. Ni vema kilichofanyika kikaangalia rasilimali zote za nchi hii na sio wawekezaji wa nje tu hata wa ndani.

Kwa mfano Tanzanite iko Tanzania pekee lakini biashara ifanyike Nairobi na New Delhi haya ni mambo ya msingi kuyaona na kuyafatilia.
  
Wito wangu kwa viongozi inapokuja suala la rasilimali za taifa tuwe na uongozi wa kitaifa sio chama wala taasisi, wala kukumbusha lipo ovu au baya lililofanyika Tanzania kwanza Mungu ibariki Tanzania Mungu Mbariki Rais wetu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages