Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya hapa nchini, Kifaru Motors (T) kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo, kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu kumkabidhi Makonda funguo za gari hilo lenye thamani ya sh. 55.
Meneja Liu alisema, gari hilo ambalo ni la kisasa litasaidia kwa kiasi kikubwa shughuli kwenye taasisi yoyote iliyopo chini ya Mamlaka ya mkoa huo wa Dar es Salaam.
Kwa upande wake Makonda aliwashuhukuru wahisani hao kwa msaada wa gari hilo na kuahidi kulitumia kwa lengo lililokusudiwa.
Makonda alisema, ili kutohisiwa kuwa amependelea, utaratibu wa Idara itakayotumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi.
"Nitatoa namba maalum ambayo wananchi wataitumia kutoa maoni kwa muda wa siku kumi kuchagua idara wanayoona inatija zaidi kutumia gari hilo kwa mfano Idara ya Elimu, Afya, Polisi na nyinginezo", alisema Makonda wakati wa makabidhiano hayo.
Mkuu wa mka wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea ufunguo wa gari aina ya Wingle 5, kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu, wakati wa Makabidhiano hayo, leo. Kushoto ni Mario Gasparri wa Kifaru Group ambayo pia ni mdao wa kampuni hiyo ya magari ya China.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu (kushoto), akitoa maelezo kabla ya makabidhiano. Wapili kushoto ni Brigedia Mstaafu Michael Luwongo kutoka kampuni ya Kifaru na Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisikiliza maelezo hayo.
Makonda akilitazama gari hilo kabla ya kukabidhiwa
Makonda akilijaribu gari hilo
Makonda akilijaribu gari hilo
Makonda akiagana na Brigedia Mstaafu Michael Luwongo kutoka Kampuni ya magari ya Kifaru
Makonda akiagana na ugeni mwishoni mwa makabidhiano hayo. PICHA: BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269