NA LIDYA CHURI-MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, amewataka mawakili kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi na za kimataifa ili kuweza kuwasaidia Watanzania katika masuala yanayohusu sheria hususan wananchi wanyonge ili nchi ya Tanzania iweze kufikia malengo ya kimaendeleo .
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Jaji Mkuu huyo, wakati hafla fupi ya kuwapokea na mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa kuwa mawakili, iliyofanyika leo kwenye Kiwanja cha Mahakama Kuu kilichopo jijini Dar es Salaam.
“Leo tumewaapisha mawakili waliokubaliwa, nilifanya nao mazungumzo kila mmoja, wengi wao ni vijana wadogo wenye miaka 25 hadi 30 ya kufanya kazi ya sheria. Hivyo kukubaliwa kwao sio mwisho wa kusoma wanapaswa kusoma sheria za kimataifa ili kufahamu sheria za utaratibu wan chi zingine,”
Profesa Juma aliwataka mawakili hao, hao waendelee kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia maadili na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya rushwa,kwa sababu bado wananchi wana hisia kwamba tatizo la rushwa ni kubwa ndani ya Mahakama ya Tanzania.
“Wazazi na Serikali imetumia gharama kubwa kuwasomesha, hivyo watambue watambue mchango huu, waisaidie serikali na wazazi wao ili Tanzania isonge mbele, alisisitiza Lidya Churi.
Akijibu swali lililoulizwa na baadhi ya waandishi kuhusu kuwepo kwa tetezi kwamba Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), alisema sheria ikitungwa haitalenga mtu wala taasisi, hivyo hofu hiyo haina sababu kuwepo kwa kuwa mawakili ni sehemu ya mahakama.
Your Ad Spot
Jul 1, 2017
Home
Unlabelled
MAWAKILI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI NA ZA KIMATAIFA
MAWAKILI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI NA ZA KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269