Breaking News

Your Ad Spot

Oct 9, 2017

UHURU FM YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WANAOUGUA SARATANI MUHIMBILI, LEO

 Kampuni ya Peoples Media, inayoendesha Kituo cha Radio cha Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, leo imeendeleza kampeni yake ya "Gusa maisha yao", ambayo imeianzisha hivi karibuni kwa ajili ya kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere, kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula kwenye Kituo cha kuhudumia watoto wanaougua Saratani cha Tumaini la Maisha kilichopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pichani, Meneja Rasiliamli watu wa Uhuru FM  Paul Mng'ong'o akikabidhi vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni mbili kwa Mkuu wa Kituo hicho cha watoto wenye kuugua saratani, Lilian Ndyetabura. Kushoto ni Meneja rasilimali watu wa Kiwanda cha Urafiki cha Ubungo Dar es Salaam Edwin Mkwanga ambaye alihudguria utoaji msaada huo kutokana na kiwanda hicho kuichangia Uhuru FM doti 100 za kanga. Tafadhali tazama picha nyingine zinazoendelea zikionyesha taswira mbalimbali kuhusuhafla hiyo....



































No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages