Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, akielezea jinsi huduma hiyo iyakavyofanya kazi. |
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID. ARUSHA
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amezindua huduma mpya
itakayowawezesha waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,
(WCF), kwa kutumia mtandao wa Internet.
Mhe.
Mhagama amezindua huduma hiyo leo Novemba 29, 2017, wakati wa Mkutano
wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF),
kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC,
Arusha.
“Huduma
hii itawawezesha waajiri kujisajili na Mfuko kupitia mtandao wa
internet na hawalazimiki kujaza fomu na kuja ofisini kwetu au kwa
maafuisa kazi” Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi,
alisema wakati akitambulisha huduma hiyo kwa Mhe. Waziri.
Katika hatua nyingine, Benki ya NMB Bank plc imenyakua tuzo baada ya kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi.
Kampuni
zingine zilizonyakua tuzo kundi la waajiri ni Steel Master Ltd kwa kuwa
mwajiri bora katika uwasilishaji nyaraka za madai ya fidia kwa
wafanyakazi na kampuni nyingine ni KPMG Advisory Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michango miongoni mwa kundi la waajiri wenye wafanyakazi wengi.
WCF
iliwatunukia tuzo wadau wa Mfuko huo ambapo Waziri Jenista kwa niaba ya
Serikali alipokea tuzo hiyo, kwa kutambua mchango wa Serikali katika
kuanzisha na kufanikisha utendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Wadau
wengine ni Shirika la Vyama vya Wafanyakazi, (ATE), Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi, (TUCTA), Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii,
(SSRA), kwa kutambua ushiriki wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi, (WCF)
Waziri
Mhagama (watatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.
Eric Shitindi, (wakwanza kushoro), wakipokea hundi yenye thamani ya
shilingi milioini 33.8 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
WCF, Bw. Emmanuel Humba, (wapili kushoto). Fedhab hizo ni kwa ajili ya
kusaidia ununuzi wa komputa nundu (perkins Braille Machines) kwa ajili
ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona katika shule za umma.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya WCF,. Wakwanza kushoto ni katibu wa Waziri Jenista Mhagama.
Mheshimiwa
Waziri Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Bw. Richard L.Makungwa kutoka
NMB Bank Plc tuzo ya mwajiri mwajiri bora katika uwasilishaji michngo
miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
ya WCF, Bw. Emmanuel Humba.
Mheshimiwa
Waziri akimkabidhi tuzo Kaimu Mwenyekiti wa ATE, Bi. Janet Reuben
Lekashingo tuzo ya ushiriki kama Mdau wa WCF. Anayeshuhudia ni Bw.
Humba.
Mheshimiwa
Waziri akimkabidhoi tuzo Kaimu Mwenyekiti wa ATE, Bw.Tumaini Peter
Nyamhokya, Katibu Mkuu wa TUCTA, tuzo ya ushiriki kama mdau wa WCF.
Anayeshuhudia ni Bw. Humba.
Mheshimiwa Mhagama akimkabidhi tuzo, Bw. Hiroshi Yamobana kutoka ILO kwa ushiriki na kama mdau
Waziri Jensita akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
Mwenyekiti wa Boadi ya Wadhamini ya SSRA hadi Aprili 2017, Bw.Juma Muhimbi, (kulia), akiteta jambo na Bw. Masha Mshomba
Waziri akipokea na Bw. Feddy Maro, wa AICC alipowasili mapema leo kufungua mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo, akizungumza
Kamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, na Mbunge wa Chemba, Mhe. Juma Nkamia
Bi. Sara Kibonde Msika kutoka SSRA
Mkurugenzi
Mkuu wa SSRA, Dkt. Irine Isaka akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF,
Bw. Adam Mayingu, wakati wa mkutano Mkuu wa Kwanza wa mwaka wa Wadau wa
WCF jijini Arusha Novemba 29, 2017
Mmoja wa watu wanaofaidika na Mafao ya WCF,
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269