Breaking News

Your Ad Spot

Dec 13, 2017

DK EDMUND MNDOLWA MWENYEKITI MPYA JUMUIA YA WAZAZI TANZANIA

DODOMA, TANZANIA
Mwanasiasa msomi Dk. Edmund Mndolwa (Pichani), ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi unaoelezwa kuwa wenye ushindani mkubwa uliofanyika jana, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo nje kidogo ya mji mkuu wa Dodoma.

Taarifa zimesema, katika Uchaguzi huo Abdallah Haji Haider naye pia ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo katika uchaguzi ambao Mkutano wake Mkuu mapema ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Dk John Magufuli.

Dk. Mdolwa amechukua nafasi iliyoachwa na Mwenyekiti wa zamani wa Jumuia hiyo, Alhaj abdallah Bulembo ambaye ameng'antuka baada ya kuongoza kwa miaka mitano.

Awali Bulembo alichukua fomu akitaka kutetea kiti hicho, kwa madai ya kuombwa na wadau, lakini katika hatua za mwisho alitangaza kutogombea ambapo hakuirejesha tena fomu aliyokuwa amechukua.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages