Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem (wakwanza kushoto) ameungana na mamia ya viongozi wa
Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir
Ali katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, ameungana nao kupokea na kuaga
miili ya wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha yao huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wakilinda amani chini ya muavuli wa umoja wa
mataifa. Al- Najem amesema kuwa Serikali ya Kuwait inalaani vikali tukio
la kushambuliwa wanajeshi wa Tanzania na kupelekea wanajeshi 14
kufariki huku wengine 44 wakijeruhiwa. Ameongeza kuwa' tumefuatulia
tukio hili la kushambuliwa wanajeshi wa kulinda amani katika kambi yao
huko Kongo kwa huzuni kubwa, ambapo Serikali ya Kuwait inakemea
vikali mashambulizi yanayolenga vikosi vya kulinda amani au mashirika ya kibinadamu'. hayo ameyasema
wakati wa ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar, Balozi Al-Najem amuomba Mwenyezi Mungu awarehemu wanajeshi waliouwa na kuwaponesha kwa haraka waliojeruhiwa
vikali mashambulizi yanayolenga vikosi vya kulinda amani au mashirika ya kibinadamu'. hayo ameyasema
wakati wa ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar, Balozi Al-Najem amuomba Mwenyezi Mungu awarehemu wanajeshi waliouwa na kuwaponesha kwa haraka waliojeruhiwa
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kushoto) aongoza mamia kupokea na kuaga miili ya wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha yao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakilinda amani chini ya muavuli wa umoja wa mataifa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar,
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269