Breaking News

Your Ad Spot

Dec 20, 2017

MKUTANO MKUU WAMALIZIKA DODOMA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli alipomwita mezani kwake kwa ajili ya kubadilishana mawazo wakati yakisubiriwa matokeo ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM na Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar na Bara, katika Mkutano Mkuu wa CCM uliomalizika leo jioni mjini Dodoma. Pamoja nao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Dk. Ali Mohamed Sheini
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiendelea kumsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli 
 "MKkimchagua kwa kura nyingi ndiyo mwenzenu anapata moyo.."Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete akisema wakati akitoa nasaha zake  baada ya Rais Dk Magufuli kujiuzulu Uenyekiti wa CCM kwa ajili ya kupisha uchaguzi tena wa nafasi hiyo
 Mwenyekiti wa muda wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Benjamin Mkapa akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC na Mweenyekiti wa CCM na Makamu wake wawili
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akijadili jambo na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC na Mweenyekiti wa CCM na Makamu wake wawili. Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akifuatilia
 Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM zanzibar Amani Abeid Karume akitoa nasaha, wakati yakisubiriwa matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC na Mweenyekiti wa CCM na Makamu wake wawili
 Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM Bara Mzee John Malecela akitoa nasaha, wakati yakisubiriwa matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC na Mweenyekiti wa CCM na Makamu wake wawili
 Mwandishi wa Ikulu Zanzibar Othman Maulidi akifuatilia kwa makini hali ya mambo yalivyokuwa yakienda shwari kwenye mkutano huo
 Waziri Mkuu wa zamani mwanadiplomasia mkongwe Salim Ahmed salim akitoa nasaha zake. Amesema mbali na CCM kuwa tumani kubwa Tanzania pia inatumaini sawa kwa mustakabali wa Bara la Afrika, hivyo Mwenyekiti wa CCM Dk magufuli anao pia wajibu wa kuijenga CCM yenye kuzingatia kuwa ni tegemeo pia kwa nchi nyingine za Afrika
 Waziri Mkuu wa zamani Mizengo Pinda akitoa nasaha zake
 Katibu Mkuu Mstaafu Mzee Yussuf Makamba akitoa nasaha zake. Amempongeza Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli kwa kupambana na rushwa bila aibu wa hofu 
 Mwenyekiti mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete akiongoza kuimbisha wimbo wa "tinaimani na Dk. Maguguli" wakati yakisubiriwa matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC na Mweenyekiti wa CCM na Makamu wake wawili
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitoa mwongozo wa namna ya kutangazwa matokeo katika Uchaguzi wa chama, muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC, Mwenyekiti wa CCM na Makamu wake wawili kwenye mkutano huo
 Spika wa Bunge Job Ndugai akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Wajumbe wa NEC na Mwenyekiti wa CCM na Makamu zake wawili
 Mwenyekiti wa CCM aliyekuwa amejiuzulu kupisha uchaguzi, Rais Dk Magufuli akisikiliza kwa makini wakati Ndugai akitangaza matokeo. Pamoja naye ni Mzee Mangula na Dk. Shein ambao nao walikuwa wakisubiri matokeo yao ya kuwa Makamu Wenyekiti
 Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli, Mzee Mangula na Dk Shein wakifurahi baada ya kutangazwa matokeo na wote kuibuka na ushindi wa kishondo kwa kupata kura asilimia mia kwa mia
 Mwandishi nguli wa Habari Ernest Sungura akifurahi baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa NEC 
 Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM Zanzibar Ndugu Karume akimpongeza Dk Magufuli kwa ushindi wa kishindo
 Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Kikwete kwaushindi wa kishindo
 Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Ali Hassan Mwinyi akimpongeza Dk. Shein kwa ushindi wa kishindo
 Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Kikwete akimpongeza Dk. Shein kwa ushindi wa kishindo 
 Mwenyekiti wa muda wa Mkutano huo akirejesha nyundo ya Uenyekiti wa CCM kwa Dk. Magufuli
 Mwenyekiti wa CCM Dk. Magufuli akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana baada ya kukalia tena kiti chake
 Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli akitoa neno la shukurani kwa kuchaguliwa kwa kishondo
 Baadhi ya waalikwa wakiwemo kutoka vyama vya upinzani wakimsikiliza Dk. Magufuli wakati akitoa neo la shukurani
 Wajumbe ukumbini wakishangilia
 Wajumbea na waalikwa wakishangilia ukumbini
 Wajumbe kutoka mkoa wa Kigoma wakiwa ukumbini
 Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini akihamasisha wakati kundi hilo likiimba wimbo wa kumpongeza Dk Magufuli kuibuka na ushindi wa kishindo
 Kahdia Kopa akifanya manjonjo yake wakati TOT ikiimba wimbo wa kuwaaga wajumbe
 Vijana wakiselebuka ukumbini kwa wimbo wa TOT
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli akiwaaga viongozi akiwa tayari kutoka ukumbini baada ya kumalizika mkutano wa tisa wa CCM mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli akipunga mkono kuwaaga wajumbe na wageni waalikwa kwenye mkutano huo
 Dk. Magufuli na Dk shein wakitoka ukumbini
 'NAAM MKUTANO UMEENDA VIZURI' inaelekea ndivyo walivyokuwa wakisema wakati Dk Magufuli, Dk. Shein na Ndugu Kinana wakitoka ukumbini kwenda kupanda magari kwenda kupumzika baada ya mkutano huo
 Mmoja wa wajumbe akimpongeza Mzee Steven Wassira (kulia) nje ya ukumbi kutokana na kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa NEC
Baadhi ya wasanii wa TOT wakipunga upepo nje ya ukumbi baada ya mkutano kuisha

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages