Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka umetoa washindi wa wawili wa sh. Milioni 10 katika droo maalumu ya mwisho wa mwaka ili kuwapa wachezaji wa droo hiyo kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka .
Akizungumza na waandishi habari wakati wa kukabidhi hundi hizo kwa washindi hao , Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba amesema droo hiyo inachezwa majira ya saa tatu na nusu usiku ambayo inakwenda hadi mwishoni wa mwaka.
Kemi amesema kuwa washindi wote waliopewa hundi ni kutokana na kushinda mchezo huo kwa kufuata taratibu zilizowekwa za mchezo,Amesema Watanzania waendelee kuchangamkia fursa ya mchezo huo na kuibuka washindi na kufurahi msimu wa sikukuuu na ziku zinazoendelea.
Kemi amesema kuwa droo ya walioshinda ni maalumu na wakiona umuhimu wataweza kuitumia na droo zingine zikiendelea.Mshindi wa Tatu Mzuka wa Sh.milioni 10, Samson Mwamwenda amesema hakuamini kama ameshinda kutokana na kusikia watu wanashinda.
Amesema kuwa amecheza kwa wiki mbili akipata sh.2000 na mara ya mwisho akapata sh.10,000 lakini ameweza kushinda milioni 10.
Afisa Habari wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi hundi ya
sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka ,Samson Mwamwenda,mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo
jijini Dar .
Afisa
Habari wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi hundi ya
sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka ,Godfrey Madeje,mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo
jijini Dar .
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269