Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadahan
Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imevitaka Vyama vya Siasa kusoma na kuzingatia sheria zote za Uchaguzi kabla ya kuilalamikia na kuishnikiza kufanya maamuzi ambayo ni kinyume cha Sheria.
Pia NEC imesisitiza kuwa uchaguzi Mdogo wa Wabunge na Madiwani katika Kata Sita upo pale pele na hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea hadi sasa kuelekea katika Uchaguzi huo Mdogo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwaka 2018.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani, ameiambia Uhuru FM kuwa NEC haiutambui Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA kwa kuwa hautambuliwi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini.
Kauli ya NEC, imekuja baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuahirisha uchaguzi huo vinginevyo Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA hautashiriki Uchaguzi kwa madai ya kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa Madiwani.
Akizungumzia kauli ya Mbowe, Mchambuzi wa Masuala ya Siasa Nchini Kabale Lugenzi, amesema, hatua ya vyama vya Upinzani kususia uchaguzi huo, kunawanyima haki ya Kikatiba Wanachama wanaohitaji kushiriki uchaguzi huo.
Nao baadhi ya wanachama wa vyama vya Upinzani, wamesema hatua ya viongozi wao wa juu kususia uchaguzi huo kunawapa wasiwasi katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269