Breaking News

Your Ad Spot

Feb 14, 2018

AMIRIJESHI MKUU RAIS DK. MAGUFULI ATEUA MNADHIMU MKUU MPYA WA JWTZ, AWAPANDISHA VYEO MABRIGEDIA JENERALI KUMI, LEO

IKULU, DAR ES SALAAM
Amirijeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dk John Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakub Hassan Mohammed kuwa Mnadhimu Mkuu mpya wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, pamoja na uteuzi huo amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na Luteni Jenerali  na mteule huyo anachukua nafasi aliyokuwa nayo Luteni Jenerali Aloyce Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Aidha, Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;
1.Brig Jen. J.G. Kingu,  2. Brig Jen. M.S. Busungu, 3. Brig Jen. R.R. Mrangira, 4. Brig Jen. B.K. Masanja, 5. Brig Jen. G.T. Msongole, 6. Brig Jen. A.F. Kapinga 7. Brig Jen. K.P. Njelekela, 8. Brig Jen. A.S. Bahati, 9. Brig Jen. M.E. Mkingule, 10. Brig Jen. S.S. Makona

Taarifa ya Ikulu imesema, Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ LuteniJenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages