Breaking News

Your Ad Spot

Oct 30, 2023

BABA HALISI AWASIMIKA WATEKELEZA SAUTI 300 WA KANAISA HALISI NDANI NA NJE YA TANZANIA, KAMANDA WA POLISI MTATIRO ATOA NENO

 

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi, akiwafunda Watekeleza Sauti ya Chanzo Halisi wa Kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, wakati akiwasimika kutumikia nafasi hiyo, katika Ibada iliyofanyika Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, jana, Jumapili, Oktoba 29, 2023 au 19 Buli 1Majira Halisi, kwa kalenda ya Kanisa Halisi,  Watekeleza Sauti waliosimikwa ni kutoka zaidi ya Vituo 300 vya Kanisa hilo hapa Tanzania na vituo vilivyoko Kenya, Uganda, Congo DRC, Burundi, Rwanda, Zambia, Msumbiji, Malawi na Boston nchini Marekani.

Watekeleza Sauti na Uzao wakimsikiliza Baba Halisi.
Watekeleza Sauti na Uzao wakimsikiliza Baba Halisi.
Watekeleza Sauti na Uzao wakimsikiliza Baba Halisi.
Watekeleza Sauti na Uzao wakimsikiliza Baba Halisi.

Baba Halisi akigeuza Maji kuwa Damu Safi Nyeupe ya Chanzo Halisi (Muumba) ili Chanzo Halisi mwenyewe aimiki Ibada hiyo ya kuwasimika Watekeleza Sauti. Kisha akampa nafasi mwimbaji Uelewa wa Sauti kuimbisha wimbo.

Mwimbaji Uelewa wa Sauti akiimbisha wimbo wa 'Imekuwa' na waimbaji wa Bendi ya Kanisa Halisi.
Mwimbaji Uelewa wa Sauti (ushoto) akiendelea kuimbisha wimbo 'imekuwa' huku Watekeleza Sauti, Uzao na wote wakiselebuka kwa furaha ukumbini.
Baba Halisi akiendelea kuweka 'vitu' vyake sawa kwa utulivu mkubwa wakati wimbo ukiendelea.
Baada ya wimbo 'imekuwa', Baba Halisi akainua shukurani ya kuanza Ibada hiyo ya kuwasimika watekeleza Sauti. Kisha akanza kueleza maana ya Kanisa Halisi kuwa na Watekeleza Sauti na maana ya Watekeleza Sauti.

Baba Halisi akieleza maana ya Kanisa Halisi kuwa na Watekeleza Sauti.
Baba Halisi akiendelea kufafanua maana ya watekeleza sauti na umuhimu wa wao kuwepo na wanavyotakiwa kuiishi safu ya Utekeleza Sauti.
Moja Halisi akisoma Kitabu kuonyesha uhalisia wa maneo aliyokuwa akisema Baba Halisi kuhusu maana ya Watekeleza Sauti. Karibu yake ni Faida Halisi.
Baba Halisi akiendelea kufafanua kuhusu Watekeleza Sauti. Mama Halisi akimsikiliza kwa makini Baba Halisi.

Kaka Mnara Mmoja Halisi na Dada Udhihirisho Halisi, wakimsikiliza kwa makini Baba Halisi.
Baadhi ya Wana-Safu wa Kanisa Halisi wakimsikiliza Baba Halisi kwa makini.
Mtangazaji wa Star Tv (kushoto) aliyekuwa akiendesha matangazo ya moja kwa moja ya Ibada hiyo, akimsikiliza Baba Halisi.

Baba Halisi akifurahia jambo ambalo lilitokea wakati akiendelea kufundisha kuhusu Watekeleza Sauti.
Baba Halisi akifanya shukurani ya kuwasimika Watekeleza Sauti hao.
Watekeleza sauti na Uzao wakisgangilia baada ya Baba Halisi kukamilisha Shukurani ya kuwasimika watekeleza Sauti.

Dada Utimilifu Halisi akiimbisha wimbo baada ya Baba Halisi kumaliza shukurani ya kuwasimika Watekeleza Sauti.
Dada Utimilifu Halisi (kushoto) akiendelea kuimbisha wimbo huku Watekeleza sauti na Uzao wakiserebuka ukumbini kufuarhia.
Uzao akijaribu 'kupaa' wakati akicheza kumtukuza Chanzo Halisi.
Wafanyakazi wa Star Tv wakiwa kazini kurusha moja kwa moja matangazo ya Ibada hiyo.

KUKABIDHI VYETI WATEKELELEZA SAUTI. "Sasa kwa jinsi walivyofika kwa haraka baada ya kuwaita nimeamini kuwa wana utii mkubwa kwa Chanzo Halisi, sasa kutokana na hivyo nikaona watakaowakabidhi vyeti wawe ni hawa wageni wetu kutoka Polisi, maana Polisi wanao utii wa kutosha", akasema Baba Halisi akiwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbweni Alex Bichuma aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Mtariro Kitikwi. Katikati ni Mdau wa Polisi Dk.Yatosha.

Baba Halisi akikabidhi cheti Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbweni Alex Bichuma kwa ajili ya kukabidhi Mtekeleza Sauti. Kulia ni Mdau wa Polisi Dk. Yatosha na kushoto ni Moja Halisi.

Dk.Yatosha akikabidhi vyeti Watekeleza Sauti mmoja baada ya mwingine. Cheti kilikuwa kinaanzia kwa Moja Halisi (kushoto) kwenda kwa Baba Halisi na kwenda kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbweni naye kumkabidhi Dk. Yatosha.
Baada ya hatua ya kukabidhi vyeti kukamilika Baba Halisi akafanya shukurani kisha akamkaribisha Dk. Yatosha kumkaribisha Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbweni kuzungumza.

Dk. Yatosha akizungumza na kumkaribisha Mkuu wa Kituo cha Polisi  Mbweni Alex Bichuma.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbweni Alex Bichuma akizungumza, akasema; "Polisi wanafarijika kuona viongozi wa dini wanashirikiana na jesh hilo katika kazi za kijamii, wakiamini Polisi wanafanya doria ya kimwili lakini Kanisa linafanya doria ya kiroho, hivyo kuleta maendeleo chanya kwa taifa.
 
Baba Halisi akimshukuru Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbweni kwa maneo muhimu aliyotoa.
Baba Halisi akiwakaribisha baadhi ya Watekeleza Sauti kuzungumza kwa niaba ya wenzao.

Mtekeleza Sauti wa Njombe akizunumza kwa niaba ya Watekeleza Sauti wa mikoa mingine walio waliosimikwa.
Mtekeleza Sauti wa Rwanda akizungumza kwa niaba ya Watekeleza sauti wa Mataifa ya Nje waliosimikwa.

Mtekeleza Sauti wa Kenya pia akapata nafasi ya kuzungumzia kusimikwa kwao.
 
Mtekeleza Sauti wa Uganda akizungumzia usimikwaji huo, baada ya Mtekeleza Sauti wa Mozambique (Kulia) kumaliza kuzungumza.
Moja Halisi (kulia) na Faida Halisi waimshangilia Mtekeleza Sauti huyo wa Uganda baada ya kuzungumza mazito.

Mtekeleza Sauti wa Congo-DRC akizungumza baada na yeye kupewa nafasi na Baba Halisi.
 
Mtangazaji wa StarTv (kulia), akifunga matangazo ya moja kwa moja mwishoni mwa Ibada hiyo.

Baba Halisi akinyinyiza Damu Safi nyeupe kuzunguka Utajirishoni kuhitimisha Ibada hiyo.

Baada ya bashrafu hiyo ya Matukio katika picha, msikilize Baba Halisi aliyonena akiendesha Ibada hiyo👇

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages