Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi DK Emmanuel Nchimbi leo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kigoma.
Asubuhi atafanyiwa mapokezi rasmi atakapowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma tayari kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
Baada ya kumaliza ziara ya Mkoa huo ataendelea katika mikoa mingine minne ambayo ni Geita, Kagera, Mara na Mwanza.
Lengo
la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za
wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao
na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya
maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Katika
ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na
Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi
Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg.
Rabia Abdallah Hamid.
Hivi karibuni amemaliza ziara ya siku nne yenye mafanikio makubwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269