Anaandika Nguli Yahya Msangi, Togo
Baada ya Tanganyika (Tanzania Bara) kupata Uhuru Disemba 1961 nchi ilijikutana matatizo mengi ya kijamii. Haraka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akagundua nafasi ya wasanii kukabili matatizo haya.
Leo nitakumbusha matatizo mawili na jinsi wasanii wawili walivyotumika kuyakabili kwa mafanikio makubwa mno.
1. Kanda ya ziwa kulizuka mauaji na uhujumu uchumi. Mauaji yalihusu watu wenye mwanya na wenye upara. Walitokea watu wakaaminisha wenzao ukipeleka Marekani kichwa cha wenye mwanya au upara utavuna dola kibao. Au vichwa hivi vina bahati kwenye uchimbaji madini ya almasi na dhahabu.
Japo Mwalimu alichukia sana ukabila alilazimika kutumia msanii atakayefikisha ujumbe kwa Wasukuma na Wanyamwezi kirahisi. Ndipo Mzee Mwinamila kwa maelekezo ya chama cha Tanganyika African National Unioni (TANU) akatunga wimbo. Hata kama wewe sio msukuma wala mnyamwezi utaelewa anachozungumzia maana alichanganya na Kiswahili kidogo. Usikilize.
2. Baada ya Azimio la Arusha yalianzishwa mashirika ya usafiri wa umma. Kina Co cabs (taxi za Mzizima), UDA, KAMATA na Railway Bus. Bahati mbaya madereva wakawa wakorofi. Ajali zikawa nyingi sana. Enzi madereva wakiamini mwenda kwa miguu au baisikeli au pikipiki wanapaswa kupisha bus au taxi.
Waliwaona kama watumia barabara ni wa daraja la pili. Na kweli usipotoka utagongwa. Basi haraka TANU ikamuagiza kada wake mkufunzi TANU Youth League (TYL) atunge wimbo. Kada huyo alikuwa Mzee Makongoro, akatunga wimbo ambao madereva na wasio madeeva uliwagusa sana enzi ile, ajali zikapungua.
Baadhi ya watu wanadai aliutumga wimbo baada ya yeye kugongwa. Hii si kweli. Mzee Makongoro aligongwa miaka kama miwili baada ya kutunga wimbo huo. Pia wanadai huyo dereva Hussein ndiye aliyemgonga, hii pia sio kweli kwani Hussein aliyemuimba alikuwa dereva wa UDA aliyeangusha basi jipya kwa mbwembembwe jirani na lilipo sasa daraja la Jangwani. (Link ya nyimbo ya Mzee Mwinamila: https://youtu.be/47wjM6J7hmk?si=pkYWan4Z3810iCNl)
Hawa walikuwa wazee lakini wenye akili. Waliweza kuelimisha jamii, kukemea maovu kwa kupitia sanaa
Mungu awahifadhi huko walipo inshaalah.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269