Breaking News

Your Ad Spot

Jan 10, 2010

BANGI NA TARIME, TARIME NA BANGI DUUUUUU!


MKUU wa kikosi cha kupambana na dawa za kulevya kanda maalum ya tarime na Rorya, SSP Zacharia akionyesha nyumba iliyodaiwa kukutwa na bangi
POLISI wakifyeka mashamba ya bangi katika kijiji cha Kewamamba, kata ya Nyandoto, Tarime. (Picha na
Samson Chacha).

                                     STORIIIIII
                           Samson Chacha kutoka Tarime anatonya hivi.........
POLISI WATEKETEZA TANI 5 ZA BANGI , WANAKIJIJI WATIMKA  MAKAZI KUOGOPA KUDAKWA.
Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya wameteketeza tani tano za bangi ikiwemo tani moja iliyokuwa ndani ya nyumba katika kijiji cha Kewamamba kata ya Nyandoto ,ambapo wamiliki wa mashamba na nyumba ilimokutwa wametimkia porini na milimani kuhofia kudakwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  Mkuu wa upelelezi mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya David Hiza alisema kuwa mashamba  ya bangi yalifyekwa na polisi katika kijiji hicho cha Kewamamba, Januari 6 asubuhi baada ya kutonywa na raia wema,

"Tulifika katika kijiji hicho cha Kewamamba na wananchi walipoona magari yetu walianza kukimbilia porini na kuacha miji yenyewe na tulijaribu kwenda kwa mwenyekiti wa Kijiji na Kitongoji hatukuwakuta watu miji imebaki tupu hali inayoonyesha jinsi wakazi wa kijiji hicho kinachodaiwa Kulima Bangi kwa Wingi katika kata hiyo ya Nyandoto,'' alisema mkuu huyo wa upelelezi

Alisema walifanikiwa kufyeka mashamba yenye ukubwa wa ekari 10 na walifanikiwa kukuta tani moja ya bangi kavu ndani ya nyumba ya mkazi wa kijiji hicho aliyetoroka kabla ya Polisi kuingia kwake na kuacha mji ukiwa hauna mtu,na kwamba msako huo unaendelea kote katika wilaya mbili za Tarime na Rorya ambapo mkuu huyo wa upelelezi, Bw Hiza ameshauri viongizi wa vitongoji na vijiji kusaidia kuwafichua watu wanaoshiki katika kilimo cha zao hilo haramu na kushiriki katika msako,

Vijiji vinavyotuhumiwa kwa ukulima wa zao hilo la Bangi katika wilaya hizo mbili Tarime na Rorya ni pamoja na vijiji vya Korotambe , Remagwe, Kubiterere, Nyamohonda, Matamankwi , Tagota, Ikoma , Kogaja, Kiongera , Nyabirongo , Nkongore, Ngerengere , Magena , Nyasaricho na Turugeti ,

Chacha namba yake ni hii: 0788312145,

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages