RAIS JAKAYA KIKWETERAIS Jakaya Kikwete, aliondoka nchini jana mchana kwenda Davos, Uswisi kuhudhuria kikao cha kila mwaka kuhusu uchumi (World Economic Forum).
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, jijini Dar es Salaam, kikao hicho kitakachoanza kesho na kumalizika Januari 30, mwaka huu, kinahudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi, wachumi, viongozi wa mashirika mbalimbali, wanataaluma, viongozi wa dini na wanaharakati mbalimbali duniani.
Baada ya kikao cha Davos, Rais Kikwete ataelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha Wakuu wa Nchi za Afrika, kitakachoanza Januari 31 hadi Februari 2, mwaka huu na kurejea nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269