Breaking News

Your Ad Spot

Jan 28, 2010

MREMA AENDA INDIA KUTIBIWA

MWENYEKITI  wa TLP, Augustine Mrema yuko nchini India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa kisukari. Mrema, ambaye aliondoka wiki iliyopita, atakuwa akitibiwa Hospitali ya Appollo iliyopo jijini Bambay. Kaimu katibu mkuu wa TLP, Hamad Tao alisema Mrema amekwenda India ili kukutana na wataalam wa ugonjwa huo."Amekwenda tangu wiki iliyopita na atakaa huko kwa wiki tatu ili wataalam waweze kumpatia matibabu,"alisema Tao.
Alisema kuwa huo umekuwa ni utaratibu wa Mrema, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwenda India kutibiwa ugonjwa huo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda sasa na kwamba Mrema anagharimia mwenyewe matibabu yake na kwamba hatumii fedha za TLP.

Mweeyekiti wa TLP Augustine Mrema akimuombea kura kwa wananchi mgombea wake wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Biharamulo, Juni mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages