Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2010

FOMU ZAANZA KUTOLEWA NA CCM KUJAZWA NAFASI ILIYOTEMWA NA HAJI MANARA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, kimeanza kutoa fomu kwa ajili ya wanachama kuomba kugombea nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa humo, iliyoachwa wazi na Haji Manara kutokana na kukabiliwa na kashfa. Uchaguzi umepangwa kufanyika Machi 28, 2010. Pichani, mmoja wa waliojitokeza kuchukua fomu hizo, Ofisa Masoko wa Uhuru FM, Furaha Luhende (kulia) akikabidhiwa fomu na Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Adamu Makulilo, kwenye ofisi ya mkoa, leo.
 Luhende akionyesha fomu baada ya kukabidhiwa katika ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo Hadi jioni zaidi ya wanachama 12 walikuwa wameripotiwa kuchukua fomu hizo akiwemo aliyekuwa akishika wadhifa unaogombewa, Salim Mwaking'inda aliyeng'olewa na Manara katika uchaguzi mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages