Breaking News

Your Ad Spot

Feb 2, 2010

JACOB ZUMA ATETEWA DHIDI YA SHUTUMA ZA UZINZI

Chama tawala nchini Afrika kusini ANC, kimeteta Rais Jacob Zuma (Piochabi), dhidi ya madai kuwa alipata mtoto nje ya ndoa na kuwa anaaibisha nchi kwa tabia yake ya uzinzi.
Kwa mujibu wa wakuu wa chama, bwana Zuma hajavunja sheria zozote na kwamba hakuna cha kuaibisha katika uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wawili.
     Vyama vya upinzani pamoja na vyombo vya habari vimemushutumu Zuma kwa kukiuka maadili pamoja na kutoa mfano mbovu kwa nchi inayokabiliana na ugonjwa hatari wa ukimwi.
    Mmoja wa wabunge nchini Kenneth Meshoe amemtaka Zuma kutafuta ushuari nasaha kwa tabia yake kama alivyofanya mcheza golf mashuhuri Tiger Woods.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages