Breaking News

Your Ad Spot

Feb 5, 2010

JERRY MURRO NA WENGINE WAWILI WATINGA KIZIMBANI LEO


JERRY MURRO

Mtangazaji wa TBC 1 Jerry Murro na watu wengine wawili Edmund Kapama na Deogtratius Ngassa leo wametinga kizimbani katika Mahakama ya Hakim Mkazi jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka kadhaa ikiwemo kula njama za kutaka kupokea rushwa.

Mbele ya Hakim Mkazi wa Mahakama hiyo, Gabriel Mirumbe, Murro na enzake amedaiwa kwa pamoja kuomnba rushwa  ya sh. milioni 10 kwa  aliyekuwa meka hazina wa wilaya ya Bagamoyo Michael Wage aliyefukuza kazi hivi karibni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Mwendesha mashitaka wa serikali , Boniface Stanslaus  akiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Benny Lincolin  wamedai mahakamani kwamba  mshitakiwa wa kanza na  wa pili pia wanakabilia na shitaka la kujipachika wadhifa usio wao.

Inadaiwa Januari 29, mwaka huu katika hoteli ya Sea Clif washitakiwa walijitambulisha mbele ya Wage kua wao ni maofisa wa TAKUKURU wakati sio kweli.

Upande wa mashitaka uliiomba mahakama isitoe dhamana kwa washitakiwa wa kwanza na wa pili kwa madai kwamba waliahi kufungwa na kuwa kwao nje kutaharibu upelelezi ambao bado unaendelea.

Hata hivyo hakim alipotaka upande wa mashitaka kuthibitisha kama ashitakiwa hao waliwahi kufungwa , upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hivyo ikabidi dhamana ienele kuwa wazi, kwa sharti la kila mmoja kuwa na wadhamini wa wili watakaosaini bondi ya sh. milioni 5 kila mmoja.

Jerry Murro na Edmund kapama walitimiza masharti ya dhamana  na kuachiwa huku Ngassa akipelekwa rumande hadi Februari 12, kesi itakapotinga tena mahakkamani hapo.

HABARI KATIKA PICHA
Jerry Murro akiwa chini ya ulinzi wa polisi wakati akipelekwa kizimbani.
Murro baada ya kupata dhamana.
Murro akitoka mahakamani baada ya kupata dhamana
Edmund Kapama akiondoka mahakamani baada ya kupata dhamana






No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages