Breaking News

Your Ad Spot

Feb 2, 2010

SAKATA LA JERRY MURO: WENGINE WAWILI MBARONI

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,  akiwatambulishwa watuhumiwa Edmunda Kapama (shoto) na Deogratius Ngassa akiwahusisha katika sakata la Jerry Muro, leo

STORY
Watuhumiwa wawili zaidi wakamatwa kuhusika na sakata la Jerry Muro, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inawashikiria na kuwahoji watu wawili kwa kosa la kutumia vitisho katika kudai fedha kiasi cha sh.milioni 10,000,000 kutoka kwa mlalamikaji, Michael Wage Karoli.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo mchana katika kituo ca Polisi Centre, Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Edmund Kapama mkazi wa Mwananyamala (52) na Deogratius Mgassa (35) mkazi wa Mbezi Beach.

Kova amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana katika maeneo ya Kinondoni na kabla ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao wapelelezi walifanikiwa kupata kumbukumbu za watuhumiwa hao.

Amesema kwa kutumia kifaa cha ELEKTRONIC (CCTV) chenye uwezo wa kurekodi na kutunza kumbukumbu ambapo katika tukio hilo watuhumiwa watatu walionekana wakiwa katika meza ya mazungumzo pamoja na mlalamikaji.

Kamanda Kova amesema kuwa watuhumiwa hao walifanyiwa gwaride la utambulisho na kutambuliwa na mlalamikaji, Michael Wage Karoli.

Katika taarifa yake Jeshi la Polisi imesema kuwa watuhumiwa hao wawili waliokamatwa ni matapeli sugu na hivi sasa wanakabiliwa na kesi nyingine na hivyo kukosa sifa za kupata dhamana mpaka watakapofikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Jarida la Jerry Muro limepelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuona kama ana kesi ya kujibu, na kwa mujibi wa Kamanda Kova endapo mwandishi huyo bora wa mwaka 2009 akionekana ana kesi ya kujibu ataunganishwa na hao wawili kwenye mashitaka.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages