Breaking News

Your Ad Spot

Feb 1, 2010

KATIBU MKUU WA TLP AAGA DUNIA


KATIBU Mkuu wa Chama TLP, John Komba (Pichani),  amefariki dunia katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.Komba alikuwa amelazwa akiwa amepooza mwili upande mmoja.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Hamad Rashid Thao alisema Komba alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali hiyo alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki mbili.
        Thao alisema Komba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza upande wa kulia wa mwili wake na alifikishwa hospitalini hapo tangu Desemba 27 mwaka jana.
       Alisema alitibiwa na alipata nafuu na kurudi nyumbani kwake lakini siku chache baadaye hali hiyo ilimrudia na Januari 25 mwaka alirejeshwa hospitalini hapo hadi jana alipofariki dunia.
       Kwa mujibu wa Thao, Komba atazikwa kesho(Jumatano) shambani kwake eneo la Goba, Mbezi, Dar es salaam.
    CIAO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages