Breaking News

Your Ad Spot

Feb 22, 2010

Lufthansa wagoma

Shirika la ndege la kitaifa la Ujerumani, Lufthansa, limelazimika kusitisha safari zake baada ya marubani wake wote kuanza mgomo wa siku nne kuhusu mishahara na usalama wa kazi zao.


Shirika hilo limesimamisha zaidi ya safari 3,000 za ndege zao. Msemaji wa shirika hilo Klaus Walther amesema mgomo huo utailetea kampuni hasara ya zaidi ya dola milioni 136.

Chama cha marubani hao, Cockpit, kimesema kinataka wanachama wake kupewa nyongonza ya mshahara ya asilimia 6.3.

Pia kinataka Lufthansa kuwahakikishia marubani wake kuwa hawatapoteza kazi wakati ambapo kampuni hiyo itaanza kutumia makampuni mengine ya ndege kutoa baadhi ya huduma zake.

Vilevile chama hicho kinataka kupewa nafasi ya kuchangia zaidi katika maamuzi yanayofanywa na kampuni hiyo. Hadi sasa pande hizo mbili hazijaafikiana kufanya mazungumzo, lakini Klaus Walther anasema Lufthansa iko tayari kufanya hivyo.



http://www.bbcswahili.com/

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages