Breaking News

Your Ad Spot

Feb 22, 2010

WAMBURA WA ENZI ZA FAT AVIKWA UKAMANDA WA VIJANA SINZA

WANAHAMASA wakiserebuka kwenye viwanja vya Ofisi ya CCM, Kata ya Sinza wakati wa kutawaza Kamanda wa Kata hiyo  na wa matawi, jana.
MJUMBE wa NEC Taifa CCM,  Nape Nnauye akimvisha joho, Mary  Shirima kuwa Kamanada wa tawi la Vijana  wa CCM  Sinza CNnauye akimvisha joho Godfrey Chikandamwali kuwa Kamanda wa tawi la Sinza DNnauye akimvisha joho Zitta Kapalata kuwa Naibu kamanda tawi la Sinza E
Nape Nnauye akimvisha joho Goodluck Mmari 'Meeda' kuwa kamanda tawi la Sinza AMJUMBE wa NEC CCM Taifda Nape Nnauye akimvisha joho aliyekuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa Chama Cha Soka Tanzania (FAT) Michael Wambura kuwa Kamanda wa UVCCM Kata ya Sinza, katika hafla iliyofanyika juzi katika ofisi ya CCM kata hiyo mjini Dar es Salaam.
 
Nauye akicheka na Nape kuvishwa joho
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Nape Nnauye (wanne kulia) akiwa na Makamanda wa Kata na matawi ya CCM Kata ya sinza, Dar es salaam, baada ya kuwatawaza katika sherehe iliyofanyika jana, kwenye ofisi ya CCm ya kata hiyo. Watatu Kushoto ni Kamanda wa Kata hiyo, Michael Wambura. Wenginbe kushoto ni Zitta Kapalata (Sinza D), Mary Shirima (Sinza C) na kutoka kulia ni Dk Alphonce Kyessy (Sinza B), Godfrey Chikandamwali (Sinza D) na Goodluck Mmari Mzee wa Meeda ya Sinza.

STORI
NA Chachandu Daily, Sinza

MAKAMANDA wa Umoja wa Vijana wa CCM nchini wametakiwa kuwasaidia vijana wa Umoja huo kuwa na vyanzo vyao mapato.
      Hayo yalisemwa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa, Nape Nnauye aliposimika makamanda wapya wa Umoja wa Vijana wa CCM katika Kata ya Sinza mjini Dar es Salaam.
     Alisema, kuwa na miradi yao ndiko kutawafanya Vijana hao kujikwamua wenyewe kila wanapopatwa na matatizo, badala ya kulazimika kuwasaka makamanda ili wawezeshe kutatua matatizo hayo, jambo ambalo linawafanya kuwa tegemezi kwa makamanda hao.
  " Hatutaki muwe mnatupatia misaada pale tunapokuwa na shida tu, badala yake tusaidieni kuwa na vyanzo endelevu vya mapato, tunapokuwa na shida tujisaidie wenyewe", alisema Nnauye.
   Aliwataka Makamanda kutumia uzoefu,kuwawezesha vijana wa CCM kupita katika njia nzuri kila wakati katika ujenzi wao wa Chama, kwa kuwa ndiyo moja ya malengo ya kuwepo Makamanda hao.
   Nnauye aliwataka Makamanda kutojiingiza katika fikra anbazo baadhi wanazo kwamba wadhifa huo ni ngazi ya kupata uongozi au maslahi binafsi na kuonya kuwa makamanda watakaoonekana kuwa na lengo hilo watavuiw mara moja ukamanda huo.
   Hata hivyo, alisema, kama wanachama wengine makamanda pia wanaruhusiwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na serikali lakini ni kwa kufuata misingi na utaratibu unaokubalika.
    Aliwataka vijana wa CCM kata hiyo ya Sinza kuwa tayari kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, kwa kutobali kupoteza haki yao ya kupata kiongozi bora badala yake wawe mstari wa mbele kuhakikisha CCM inapata wagombea safi na wenye uwezo wa kuileleta CCM ushindi dhidi ya wagombea wa upinzani.
    Katika hafla hiyo iliyotanguliwa na uzinduzi wa matawi la UVCCM,  Nape alimsimika Michael Wambura kuwa Kamanda wa Vijana Kata ya Sinza. na makamanda na manaibu wao wa matawi  matano ya UVCCM katika kata hiyo. Wanbura ni yule aliyekuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa chama cha soka Tanzania (FAT).
 Wale wa matawi ni, Goodluck Mmari 'Meeda' (Sinza A), Dk. Alphonce Kyessy na Naibu wake Suddi Ibuma (Sinza B), Mary Shirima na Naibu wake Peter Mpongole (Sinza C), Godfrey Chikandamwali (sinza D) na Gilbert Sampa na Naibu wake Zitha kapalata (Sinza C).



mwisho.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages