Breaking News

Your Ad Spot

Feb 3, 2010

SHEIKH YAHAYA HUSSEIN ATABIRI KUTOFANYIKA UCHAGUZI MKUU 2010

                                                            Sheikh Yahaya Hussein.

MNAJIMU maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein ametoa tena utabiri wake na akisema uchaguzi mkuu utakaohusisha madiwani, wabunge na kiti cha Urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautafanyika kutokana na sababu mbalimbali.

Utabiri huo alioutoa  wakati akizungumza kwenye kituo kimoja cha cha luninga unafuatia ule uliozua utata mkubwa miongoni mwa wanazuoni ambao ulisema mtu atakayejaribu kupingana na Rais na Jakaya Kikwete kwenye kinyanganyiro cha Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi atakufa kifo cha ghafla.

Akifafanua kuhusiana na utabiri wake huo Mnajimu Sheikh Yahya alisema, hataki kutoa sababu zaidi ya utabiri wake huo ili kuondoa minong’ono baina ya Watanzania ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kujadili utabiri wake na kuzua mijadala mizito miongoni mwa wanasiasa.

“Kama nilivyosema na kutabiri awali kwamba atakayepingana na Kikwete atakufa ghafla basi sasa nasisitiza kwamba, uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautafanyika na jamii itakuja kufahamu sababu zake hali ya mambo itakapojiri,” alisema Sheikh Yahaya Hussein.

Hivi karibuni Mnajimu huyo aliibua mijadala mizito kutokana na kutoa “hoja mufilisi” katika kipindi cha mwaka jana baada ya kutabiri kifo cha ghafla cha mtu atakayepingana na Jakaya Kikwete kwenye kinyanganyiro cha Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Wanaharakati wengi walitoa maoni yao kutokana na utabiri huo hali iliyochangiwa na Sheikh Yahaya Hussein kutokueleza kwa kina kuhusu wakati hasa mtu huyo mwenye kutaka urais kwa tiketi ya CCM atakapokufa ghafla.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages