Breaking News

Your Ad Spot

Mar 18, 2010

MAADHIMISHO YA 22 YA WIKI YA MAJI KITAIFA, KIBAHA

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza akitazama darubini ya kutambua aina ya mbu wenye kuambukiza malaria alipotembelea banda la Concern, kwenye maonyesho ya maadhimisho ya 22 ya wiki ya Maji kwenye viwanja vya Mwendapole Kibaha mkoa wa Pwani jana. NAIBU waziri wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza akikagua bwala linalotoa maji kwenye mradi wa kilimo cha umwagiliaji aliozindua jana katika kijiji cha Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani. Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo, Magesa Murongo NAIBU Waziri wa Maji na umwagiliaji Christopher Chiza akisaidiwa kupanda moja ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji, wakati akikagua mradi huo baada ya kuuzindua jana katika eneo la Msoga,wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani 


KINA MANA wa Jamii ya wafugaji wakimweleza Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza (wapili kulia) namna ambavyo walitaka birika la kunyweshea mifugo liwe, alipozindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji ambao pia utawapatia waugaji huduma ya kunywesha mifugo, katika kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani. WADAU wakiwa kwenye semina kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya amaji, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 22 ya wiki ya Maji . semina hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Njuweni Kibaha mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages