Breaking News

Your Ad Spot

Mar 18, 2010

WIKI YA MAJI KIBAHA, WAZIRI ATAKA WAFUGAJI WAGUSWE KATIKA UANZISHWAJI MIRADI YA SKIMU ZA UMWAGILIAJI

Kina mama wa Kimasai wakimweleza Naibu Waziri jinsi wangependa lijengwe eneo la unyweshaji maji

STORI
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Chrisopther Chiza ametaka inapoanzishwa miradi ya Kilimo cha umwagiliaji iwalenge pia wafugaji katika maeneo husika.
     Chiza alisema hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika kijiji cha Msoga wilyani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji yanayoendelea nchini kote, ikifanyika kitaifa katika mkoa huo.
    Alisema, kuwalenga kwa kuwawekea maeneo kama ya kunyeshea mifugo yao wakati wa kuanzishwa miradi hiyo kutasaidia kuondoa migongano isiyo ya lazima ambayo imekuwa ikitokea baina aya wakulima na wafugaji.
     Katika mradi huo wa Msoga, wafugaji wamelengwa kwa kujengwa eneo la birika la kunywesha mifugo ambalo ni la kisasa.
     Kuhusu mradi huo, Chiza aliwata wataalamu wa kilimo cha umwagilaji wanatoa elimu kwa wakulima ili maji ya bwawa hilo yaweze kutumika kwa utalaamu. Katika kusisitizi suala hilo alisema elimu ya shamba darasa itolewe, pia kwa wale wakulima waliopata elimu Mkindo wafundishe wenzao.
     Alizitka kamati za maendeleo ya kata kusimmmia matumizi ya maji kwa wakulima na wafugaji ili kuepusha migongano na kuagiza  utafiti ufanyike na matokeo yake yatpatikane ili shughuli za maji na kilimo ziwe endelevu.
    Kaimu Mkurugenzi wa Halimshauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Fidedelica Myovella, ambaye ni Ofisa Kilimo, mifugo na Ushirika alisema wa mradi huo ambao utagharimu sh. bilioni 2.8, unahusisha ujenzi wa bwawa na birika la kunyweshea mifugo ambalo litagharimu sh. bilioni1.9, ambapo ni awamu ya kwanza .
   Alisema awamu ya pili ni ujenzi wa miundombinu ya umwagliaji itakayogharimu sh. milioni 879, ambao unahekta 150 utawanufaisha wakulima 200 katikakilimo cha mbogamboga mfano za majani ambazo ni nyanya, bamia, matikiti maji, matngo, pilipili hoho, kabichi, mahindi na mpunga wakati wa masika.
    Myovella aliongeza kuwa mradi huo, bado unahaitaji sh. bilioni 1.4 iliuweze kukamilika kama ulivyopangwa. Pia unahitaji sh. milioni 105 ikiwa ni ombi maalum kwa ajili ya uchimbaji wa kisima kirefu na mitambo ya uzalishaji maji kutoka chini ardhi ili kuweza kutosheleza mahitaji ya maji katika eneo hilo.
    Alisema kiasi cha fedha cha sh. miloni 527.9 kinadiwa na mkandarsi wa ujenzi huo ambaye ni SUMA JKT licha ya kuukamilisha vizuri mradi huo.
       Akizungumzia kuhusu fedha hizo, Chiza alisema fedha hizo zitafutwa na kuwashukuru SUMA JKT kwa kustahimili kufanya kazi nzuri ya kukamilisha mradi huo licha ya kwamba haitalipwa fedha zote.
      Mradi huo umejengwa kupitia fedha zilizotolewa na Mfuko wa Msaada wa chakula wa Serikali ya Japan(FACF) NA Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaj wa Wilaya(DIDF),.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages