Breaking News

Your Ad Spot

Mar 17, 2010

MAADHIMISHO YA 22 YA WIKI YA MAJI KITAIFA YAPAMBA MOTO KIBAHA


NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi, Christopher Chiza akizindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Mwangomole katika kijiji cha Kwala wilayani KIbaha mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kibaha Hajat, Halima KIhemba.Bwala wa Mwangomole linalotoa maji katika mrafi huo.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa  kampuni ya  Enrweb pre pay Africa Limited, Gaston Mrancis kuhusu mita za kisasa za maji za kulipia kabla, alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya teknolojia, na huduma mbalimbali za utoaji hufuma ya maji OFISA Uhusiano wa Shirika la Maji mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani ya mkoa wa Pwani (DAWASCO), Mary Lyimo akimweleza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza kuhusu huduma zitolewazo  na kampuni hiyo, Waziri alipokagua banda la DAWASCO katika Maonyesho ya Maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji katika Viwanja vya Mwendapole,  Kihaba mkoa wa Pwani.OFISA wa Wizara ya Maji, Nyabaganga Taraba, akimweleza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza kuhusu huduma zitolewazo na kampuni hiyo, Waziri alipokagua banda la wizara hiyo katika Maonyesho ya Maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji katika Viwanja vya Mwendapole, Kihaba mkoa wa Pwani.WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza akifungua Maadhimisho ya 22 ya Wiki ya Maji na Maonyesho ya huduma na teknolojia kuhusu maji, kwenye viwanja vya Mwendapole,. Kibaha mkoa wa Pwani.WASANII wa kikundi cha kwaya kutoka Kibaha mjini wakitumbuiza katikauzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages