Breaking News

Your Ad Spot

Mar 13, 2010

BREAKING NEWS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, MELI NYINGINE YAWAKA MOTO ZENJI LEO

Meli ya MV Serengeti ikiungua moto ikiwa iko nje kidogo ya bandari ya Zanzibar jana, huku wafanyakazi wa shirika la bandari zanzibar kwa kushirikiana na kikosi cha zimamoto na uokozi(KZU) wakiwa katika jitihada za kuuzima moto huo. Meli hiyo yenye namba za usajili IMO:6818796 ilikua katika matayarisho ya kwenda kisiwani pemba. Juhudi hizo zilifeli ila hakuna maafa yaliyotokea na hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana. Usafiri wa kwenda na kutoka Pemba sasa umewekwa njia panda maana MV Serengeti ilikuwa tegemeo la wengi na haijulikana itakuwaje baadaa ya hapo
NA KHATIBU SULEIMAN, ZANZIBAR
Moto uliozuka ghafla umeiteketeza meli ya MV. Serengeti katika Bandari ya Malindi ilipokuwa ikijitayarisha kwa safari ya kwenda Pemba, leo.
     Kazi za kuokoa baadhi ya mali zilizokuwa ndani ya meli hiyo ilifanyika sambamba na kuzima moto huo.
Juhudi za kuuzima moto huo zilifanywa kwa kutumia boti mbili za Shirika la Bandari la Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya Zimamoto.
     Chanzo cha moto huo hakijulikani, ambapo katika eneo la bandari watu walijazana kushuhudia jinsi ya meli hiyo ilivyokuwa ikiteketea.
     Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi alikuwa mmoja wa viongozi waliofika sehemu hiyo kushudia tukio hilo. Abdallah alisema hasara kubwa ilisababishwa na moto huo ikizingatiwa kuwa meli hiyo ilikuwa tegemeo la watu wanaofanya safari kati ya Pemba, Unguja na Tanzania Bara.
    " Hii ni hasara kubwa, kwani meli hiyo ni moja ya mategemeo makubwa ya wananchi wanaofanya safari za kisiwa cha Pemba. Chanzo cha ajali hiyo ni mapema sana kwa sasa.....tunafanya uchunguzi kujua chanzo chake na hatujui, " alisema Msajili wa Meli Abdallah Mohamed.
    Katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichopita, wajumbe mbalimbali waliiomba serikali kuifuatilia meli hiyo kutokana na tabia ya kubeba abiria kupita uwezo.
    Meli ya Mv. Serengeti inao uwezo wa kuchukua tani 100 za mizigo na abiria 1,000 na ni maarufu kwa safari za kwenda katika kisiwa cha Pemba kiasi ya kupachikwa jina la mkombozi wa kisiwa hicho.
     Hiyo ni ajali ya pili ya moto kwa vyombo vya baharini mjini hapa, ambapo mwaka jana Meli ya MV. Aziza iliteketea kwa moto ikiwa nchi kavu kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.

3 comments:

  1. varcevanje denarja [url=http://www.mladipodjetnik.info]mladi podjetnik[/url]

    ReplyDelete
  2. varcevanje za pokojnino [url=http://www.zivljenjskozavarovanjee.info]zivljenjsko zavarovanje[/url]

    ReplyDelete
  3. Best Girls For All . [url=http://ezine.articlestrove.info/?p=95340]ezine.articlestrove[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages