Breaking News

Your Ad Spot

Mar 30, 2010

KILI TAIFA CUP YAZINDULIWA LEO, KUANZA KUTIMUA VUMBI MEI

MICHUANO ya soka ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup' mwaka huu itashirikisha pia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 (U20).
   Hayo yalisemwa jana mjini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela katika uzinduzi rasmi wa mashindano hayo,kwenye Klab ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni wadhamini kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
   Alisema wanatakaounda timu ya U20 itakayoshiriki michuano hiyo ni vijana waliovuka umri wa miaka 18, na kwamba timu hiyo inashiriki kama mchagizaji tu kwa kuwa hata ikiibuka kuwa mshindi wa kwanza haitazawadiwa.
   "mwaka huu tumeamua kushirikisha timu hii (U2) kuwezesha timu hii kujiandaa na michuano ya kimataifa ijayo,na ikiwa wataibuka na ushindi timu itakayokuwa ya pili dhidi ya tumu hiyo ndiyo itakapata zawadi ya mshindi wa kwanza", alisema Mwakalebela.
   Alisema, mashindano yatanza Mei 8 na zitashirikishwa timu 24 zitakazocheza katika vituo sita abapo kila timu itacheza na mwenzake kwenye ngazi za mzinguko kisha zitakazopata poiti nyingi zaidi zitaingia kwenye hatua ya robo fainali.
   Mwakalebela alivitaja vituo sita zitakakorindima mechi hizo kuwa ni Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga na kuwamba robo fainali zitachezwa Mei 22, 2010 na fainali zitakuwa Mei 30,2010.
   Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni bia Tanzania (TBL) David Minja alisema, TBL imedhamini michuano hiyo kwa gharama ya sh. milioni 850, tangu maandalizi ya timu hadi zawadi za washindi.
  "Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kilimanjaro Premium Lager, moja ya aina za bia za TBL kudhamini mashindano haya yanayosaidia kung'amua na kukuza vupaji mbalimbali kuanzia ngazi za chini hadi timu ya taifa", alisema Minja.
   Alisema, zawadi katika kwa washindi wa michuano huyo zitakuwa nono,lakini akasema ni mapema kutaja viwango vyake.
    Minja alisema mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa dhima ya kufikisha Tanzania kwenye kilele cha mafanikio katika medali ya mchezo wa soka.
MENEJA Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), David Minja (wapili Kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela wakizindua  mashindano ya  Kombe la Taifa (Kili Taifa Cup), leo kwenye Klab ya TBL, Ilala, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe na kulia ni Ofisa Habari wa TFF Florian Kaijage.
  

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages