BAADA ya kujengwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packes nyakati zile Tanganyika inapata Uhuru, kiwanda hicho kilihitaji kupata ng'ombe kutoka sehemu mbalimbali ya nchi.
Ng'ombe hao baadhi walifikishwa kwa malori maalum lakini wengine waliswagwa hadi eneo hilo la kiwanda ambako kulikuwa na eneo kubwa la kulisha.
Ndipo eneo walikopita ng'ombe pakaitwa 'COW WAY' na waswahili inasemekana wakawa hawawezi kusema neno hilo la kimombo wakawa wakaamua kusema KA WE yaani KAWE na kusababisha jina hilo kudumu japo kiwanda kimeshakufa kwa kuwa sasa kimebakaia amagofu tu.
Njia yenyewe walikokuwa wakipitishwa ng'ombe ni hii (kulia) ambayo sasa imefungwa kupitwa na raia kwa amri ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya Diwani wa Kata ya Kawe, Mstahiki Londa kuanzisha pilikapilika za kupitisha katapila kwenye eneo hilo akitaka iwe barabara? ya kutumiwa kwa magari badala ya waenda kwa miguu kama ilivyokuwa ikitumiwa miaka mingi iliyopita.
Your Ad Spot
Mar 23, 2010
Home
Unlabelled
NJIA YA 'COW WAY' ILIYOZAA JINA LA KAWE YAFUNGWA NA JESHI DAR
NJIA YA 'COW WAY' ILIYOZAA JINA LA KAWE YAFUNGWA NA JESHI DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Female Nude Celebrities - Newest Celebrity Porn Videos. [url=http://passivearticles.info/celebrity-stolen-clips.html]passivearticles.info/celebrity-stolen-clips[/url]
ReplyDelete