.

AFRIKA KUSINI 'WAKANYAGANA' KUNUNUA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA

Apr 16, 2010

 Maelfu ya washabiki wa soka wa Afrika Kusini, usiku wa kuamkia Alhamisi walikuwa katika misururu mirefu kwenye maduka makubwa wakitafuta nafasi ya kukata tiketi 500,000 zilizokuwa hazijauzwa kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Fifa iliafiki siku ya Jumatano kutengua uamuzi wa mauzo ya tikiti kutafanywa kwa njia ya mtandao au kupitia utaratibu kibenki.
Kwa sasa kuna uwezekano wa kupatikana tikiti kwa michezo yote, ukiwemo mchezo wa fainali katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg tarehe 11 mwezi wa Julai.
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 64 alikufa kwenye foleni mjini Cape Town huenda kutokana na uchovu akisubiri kukata tikiti.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya Africa Andrew Harding amesema kulikuwa na hali ya taharuki maeneo ya Sandton, kaskazini mwa Johannesburg, ambapo watu walikuwa wamepiga kambi mitaani usiku kucha.
         Raia wengi wa Afrika Kusini walilalamikia mchakato wa awali kwa tikiti kuuzwa kupitia mtandao wa Fifa au utaratibu wenye utata wa kura katika matawi ya benki, hali iliyoonesha kuwatenga wasio na uwezo wa kuingia kwenye mitandao, kadi za benki au kuweka pesa mapema kwa ajili ya kulipia tikiti mwezi mmoja kabla.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª