Breaking News

Your Ad Spot

Apr 6, 2010

JK AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT ndani

Husna Mwilima
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwahamisha na kuwapangia vituo vipya kama ifuatavyo:-
                     1. Gishuli M. Mbegesi - Njombe amepangiwa kwenda Kilindi
                     2. Leonidas T. Gama - Mbeya amepangiwa kwenda Ilala
                     3. Frank A. Uhaula - Tarime ameoangiwa kwenda Kiteto
                     4. Sarah Dumba - Kilindi amepangiwa kwenda Njombe
                     5. John B. Henjewele - Kiteto amepangiwa kwenda Tarime
                    6. Rashid M. Ndaile - Chunya amepangiwa kwenda Mkinga
                    7. Evans Balama - Ilala amepangiwa kwenda Mbeya
                    8.Florence A. Horombe -Bukombe amepangiwa kwenda Nzega
                    9. Zainab Kwikwega -Kasulu amepangiwa kwenda Makete
                  10 Hawa Ngh’umbi -Makete amepangiwa kwenda Bukombe
                  11. Lt. Col. John Mzurikwao -Mpanda amepangiwa kwenda Sumbawanga
                  12. Bi Betty Machangu -Nzega amepangiwa kwenda Kasulu
                  13. Dk. Rajab Lutengwe -Ulanga amepangiwa kwenda Mpanda
                  14. Francis Miti -Tandahimba amepangiwa kwenda Ulanga
                  15. Deodatus Kinawiro -Mkinga amepangiwa kwenda Chunya
Taarifa ya uteuzi huo iliyosainiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),  Aggrey Mwanri imesema pamoja na mabadiliko hayo, Rais Kikwete pia amemteua Bibi Husna Mwilima aliekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kuchukua nafasi ya Ndugu Francis Miti ambaye anahamia wilaya ya Ulanga.
     Aidha, Rais Kikwete ametengua uteuzi wa Bw. Thobias M. Sijabaje ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kutokana na kutosimamia vizuri zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo za kilimo katika wilaya ya Sumbawanga katika msimu wa mwaka 2009/2010.
    Mabadiliko haya yanakusudia kuongeza ufanisi wa kazi, kuimarisha utendaji katika wilaya hizo na yanaanza mara moja.
                                                       
                                                          Imetolewa na:

                                                  Ofisi ya Waziri Mkuu,
                                                       S. L. P. 3021
                                                     DAR ES SALAAM


                                                 Jumanne, Aprili 06, 2010.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages