.

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA MPOOOOO!!!!

Apr 6, 2010

Bashir, mimi ni mmoja wa wadau ambao hutembelea blog hii karibu kila siku. naomba uitoe hii picha ya hili tangazo ili niweze kuona maoni ya wenzangu kuhusu matangazo kama haya, maana nionavyo mimi, yanadhalilisha taifa letu na kuonekana ni watu ambao 'Tunadanganyika sana",  na pia nauliza hivi kwanini wale wanaosimamia harakati za kina mama hawachukui hatua kupinga matangazo kama haya ambayo pia yanadhalilisha wanawake?, Tena Bashir naomba kujua, hivi si kuna Tasisi inayosimamia kuhakikisha vyakula na dawa zinazotangazwa au kusambazwa kwa walaji zina ubora na salama kwa afya?.

====
Naam, nakubnaliana na wewe mia kwa mia. inaonekana kuenea kwa matangazo kama haya mitaani kuna watu ambao bila shaka wamelala kidoooogo katika utendaji. ngoja tutawauliza hawa Malmaka ya Chakula na Dawa watuambie:
Bashir

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช