.

MWANAMUZIKI WA NIGERIA KUTINGISHA DAR KESHO

Apr 19, 2010

MWANAMUZIKI kutoka nchini Nigeria,  jay Martin anatarajaiwa kuwasili leo nchini kwa ajili ya onyesho la wazi lamuziki litakalofanyika kesho katika jengo jipya la Kampuni ya Simu za mkononi ya Zain, Kinondoni Morocco jijini Dar es Salaam.
   Costantine Magavilla wa Zain alisema leo asubuhi kwamaba pamoja na mwanamuizki huyo watakuwepo pia wanaamuziki wa kizazi kipya wa hapanchini kina Chi Benz, Belle One na wengine kibao, huku kukiwa na viongo mbalimbali vya kustukiza.
   Alisema, watu zaidi ya 400 wataweza kuona onyesho hilo ukumbioni na pia litakuwa live katika moja ya luninga.
   Kwa mujibu wa Magavilla onyesho hilo ni la kuwaburudisha wateja wa Zain na wengine watakaipenda kufika kuliona ukumbini au kwenye luninga na hakuna malipo kwa watakaokwenda ukumbini.
Costantine Magavilla akizungumziaa onyesho hilo leo. Kushoto ni Tunu Kavishe pia wa Zain.Waandishi na wapigapicha za habari kwenye press conference hiyo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª