.

MZEE WA CHACHANDU-DAILY AOKOTA SIMU NA KUIKABIDHI KWA ALIYEPOTEZA

Apr 2, 2010

Bashir, Mtayarishaji wa Blog hii ambaye pia ni Mpigapicha Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Burudani ambayo huchapishwa na kampuni ya  Uhuru Publicatios Ltd,  kimkabidhi simu ya mkononi, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Tumaini, Dar es Salaam, Julieth Mushi nje ya jengo la  Millenium Tower, Kijitonyama, Dar es Salaam, jana mchana.
Mwanafunzi huyo aliangusha simu hiyo ya aina ya Nokia katika daladala  wakati walipokuwa wakisafiri na kuketi 'siti' moja Bashir, ambapo  Jully alipanda saladala hiyo eneo la Bamaga wakati ikienda Kariakoo, huku akiwa ameongozana na mwenzake na  wakatelemka Kituo cha Kinondoni
B, kwenda Chuoni.
     Baada ya wanafunzi hao kutelemka, Bashir aliiona simu hiyo ikiwa kwenye siti na kuiokota na kisha kuihifadhi bila kuizima hadi alipopigiwa na mwanafunzi huyo kupitia simu ya rafiki yake  Doris Valentine (wapili kulia) baada ya nusu saa hivi tangu washuke.
   Bashir alipokea simu  na kumhakikishia Julieth kuwa asiwe na wasiwasi atamtunzia simu hiyo hadi kumkabidhi.
   Baada ya kuhakikishiwa atapata simu yake, mwanafunzi huyo aliomba Bashir amtunzie bila kuizima simu hiyo, yeye anakwenda kufanya mitihani kwanza chuoni na atamtafuta baadaye.
   Kiasi cha saa 6 mchana, Jully alipiga tena simu  mawasiliano  ndipoendelea hadi walipokutana kwenye jengo hilo na kumkabidhi simu hiyo ambapo Jully alionekana kufurahi zaidi na kutoamini imani ya Bashir jambo lililomfanya kubaki akimkodolea macho mara mbilimbili.

Je una maoni gani kuhusu tukio hili?

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช