Breaking News

Your Ad Spot

Jan 20, 2012

NAPE ATUNUKU VYETI KATIKA MAHAFALI YA SHULE ALIKOSOMA MWANZA

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikaribishwa na Mkuu wa shule ya sekondari Nsumbi, Mwanza leo alipowasili akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape NNauye akikagua moja ya mabweni ya shule hiyo kabla ya kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari Nsumbi, Mwanza leo. Bweni hilo analokagua ndilo alitumia aliposoma kidato cha nne katika shule hiyo mwana 1994 hadi 97. Wapili kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.
 Nape akikagua ujenzi wa jengo jipya katika shule hiyo.
  Nape akikagua leo bweni alimokuwa akilala wakati anasoma kidato cha nne katika shule ya Nsumbi, Mwanza mwaka 1997.
 Nape akiwasalimia wahitimu wa kidato cha sita waliokuwa wakimsubiri awatunuku vyeti katika mahafali ya shule ya sekondari ya Nsumbi, Mwanza. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Jozephat Zakeo.
 Nape akiwa na viongozi wa shule wakiwa wamsimama kuwakumbuka wanafunzi wawili wa kidati cha sita waliofariki dunia hivi karibuni.
 Wahitimu wa kidato cha sita wakiingia kwa wimbo maalum kwenye ukumbi wa sherehe za mahafali yao.
 Wahitimu wakishangilia hotuba ya Nape.
 Wahitimu wa kidato cha tano wakiimba kuwaaga wenzao wa kidato cha sita.
 Wahitimu wakicheza ngoma ya Kisukuma.
 Nape akimzawadia Rozi Mhando mdogo, Tatu Kesi (11) baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa nyimbo za mwinbaji wa muziki wa Injili, Rose Mhando wakati wa mahafali hayo.
 Tatu Kesi (11) maarufu kama Rose Mhando mdogo, akikusanya fedha alizotuzwa na mashabiki baada ya kuimba wa ustadi mkubwa nyimbo za Mwanamuziki wa Injili Rose Mhandi kwenye mahafali hayo.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo Busagi, katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Jumla ya wahitimu  374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni  Mkuu wa shule hiyo  Josephat Zakeyo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari ya Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane na kumi) Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo. Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika shule hiyo hadi kidato cha nne ambacho alimaliza mwaka 97. Watatu ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages