.

SAFARI ZA NDEGE ZAANZA TENA ULAYA

Apr 20, 2010

Siku sita baada ya vikwazo vya usafiri wa ndege kuwekwa kaskazini mwa bara ulaya, kufuatia jivu linalotokana na mlipuko wa volcano nchini Iceland, ndege kadhaa zimerejelea safari zao.
    Ndege tatu ziliruka kutoka uwanja wa Schiphol mjini Amsterdam na kuelekea miji ya New York, Shanghai na Dubai. Shirika la ndege la Ujerumani, Lufthansa limesema, baadhi ya ndege zake zilirejelea safari zake kutoka uwanja wa Frankfurt jana jioni.
   Awali mawaziri wa uchukuzi wa nchi wanachama wa muungano wa ulaya waliafikiana kulegeza vikwazo vya usafiri wa ndege kufuatia majadiliano yaliyofanyika kwa njia ya video.
   Eneo hilo sasa limegawanywa mara tatu, moja eneo ambalo usafiri wa ndege umepigwa marufuku, pili eneo ambalo usafiri wa ndege utaruhusiwa endapo kutatokea haja na nyingine ambalo mashirika ya ndege yako huru kutumia wakati wowote.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช