.

MAKAMU MWENYEKITI BUNGE LA CHINA ATEMBELEA BUNGE LA TZ DOM

Apr 21, 2010

NAIBU Spika wa Bunge, Anne Makinda, akimpokea katika viwanja vya Bunge, Makamu mwenyeki wa Bunge la China ( National Peoples Congress) Mhe. Yan Junqi,katika Viwanja vya Bunge leo. Makamu Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake wapo katika ziara ya siko Moja nchini ambapo anatembelea Bunge la Tanzania.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, akimsindikiza kuingia katika ukumbi wa Bunge Makamu mwenyeki wa Bunge la China ( National Peoples Congress) Mhe. Yan Junqi (kulia) mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Bunge leo. Makamu Mwenyekiti huyo yupo katika ziara ya siko Moja nchini ambapo anatembelea Bunge la Tanzania.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge la watu wa China Mhe. Yan Junqi ( wa pili kushoto) akifuatilia kipindi cha maswali na majibu katika ukumbi wa Bunge Dodoma leo. Mhe. Junqi yupo katika ziara ya siko Moja nchini ambapo anatembelea Bunge la Tanzania kujionea mambo mbalimbali.
 Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta (wa tatu kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo baina ya Ujumbe wa makamu Mwenyekiti wa Bunge la china Mhe. Yan Junqi ( Mwenye Nyeupe Kushoto) katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Spika Bungeni Dodoma . Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la china , yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, ziara yake inakusudia kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania. (Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge).

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช