.

TIMU YA TAIFA POOL KWENDA UGANDA KESHO

Apr 21, 2010

* Ni kwenye michuano ya kirafiki na wenzao wa mjini Kampala
TIMU ya taifa ya mchezo wa Pool inaondoka leo kwenda Uganda kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa na timu ya taifa nchini humo.
   Akizungumza wakati wa kuaga timu hiyo, jana Makao makuu ya kampuni ya Bia tanzania (TBL) Meneja wa bia ya Safari Lager inayodhamini timu hiyo, Fimbo Butallah, alisema, michuano hiyo itafanyika mjini Kampala kwa muda wa siku tatu kuanzia Aprili 23, mwaka huu.
  Butallah alisema, TBL kuptia bia yake ya Safari Lager alisema imegharamia safari hiyo na mambo mengine ikiwemo maandalizi kwa jumla ya sh.milioni tano.
  Katibu wa Chama cha Pool cha Taifa,Amos Kafwinga alisema, hii itakuwa mara ya pili timu ya yaifa ya Pool kupambana na Uganda katika mechi za kirafiki kwa kuwa mwaka jana Ugana ilikuja nchini.
  Alisema, katika muchuano hyo ambayo ilifanyika jijini Dar es saalaam, timu ya taifa ya Tanzania ilionyesha umahiri mkubwa na kuibuka bingwa.
  "Hata hivyo Uganda ina uwezo mzuri na wachezaji wake wengi wana vipaji hivyo imetutia hamasa kucheza nao michezo mingi zaidi", alisema Kafwinga.
  Alisema, timu hiyo inaondoka nchinii na wachezaji wanane ambao kati yao wawili ni wanawake, Mwalimu na viongozi wanne.
   Kafwinga alisema baada ya kurejea kutoka Uganda timu hiyo ina mpango pia wa kwenda kucheza mechi za kirafiki katika mchi kadhaa jirani zikiwemo Kenya, Malawi na Malawi.
MENEJA wa Bia ya Safari Lager, inayotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari wakati wakuaga timu hiyoleo. Kushoto ni Rais wa Chama cha Pool Taifa, Issack TogochoButallah na Togocho wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo inayoondoka kesho kwenda Uganda
Taarifa zaidi  wasiliana na Butallah kwa
fimbo.bitallah.tz.sabmiller.com

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช