Breaking News

Your Ad Spot

May 9, 2010

KILI CUP IRINGA KUELNDELEA KESHO

BAADA ya mapumziko ya jana, michuano ya Kili Taifa Cup, itaendelea kesho katika kituo cha Iringa, kwa timu za Pinda Boys ya Rukwa Kinondoni Kombaini, Mapinduzi Stars ya Mbeya na Iringa kushuka dimbani katika mechi mbili tofauti kwenye Uwanja wa Samora mjini hapa.

Mechi iliyopangwa kuanza saa 8 mchana, itazipambanisha Rukwa na Kinondoni katika mpambanao unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa baada ya timu ya Kindondoni kushindwa kuitambia Iringa katika mechi yao jana kwa kutoka sare ya bao 1-1  na Rukwa nayo ikiwa na maumivu ya kutunguliwa  na Mbeya bao 1-0 katika juzi hiyo hiyo.

Katika mechi ya saa 10 jioni, nyasi zinatarajiwa kuumia vilivyo kwa mechi ya  Mbeya na Iringa ambao ni wenyeji itakayoonyesha ni nani zaidi kati ya timu hizo kwa kuwa kila moja ina bao moja kibindoni ambalo ilipata katika mechi zake jana ambapo Mbeya ilitungua  Rukwa  na Iringa nayo kupata sare ya 1-1 na Kinondoni.

Mchuano hiyo ambayo ni katika hatua ya makundi, timu nne zilizopo katika kituo hiki cha Iringa zinapambana ili kupata timu mbili zitakazokwenda mjini Dar es Salaam, kuungana na timu nyingine zitakazopatikana kutoka vituo vingine vitano ambako michuano hiyo inaendelea katika hatua ya makundi ambavyo ni Mwanza, Arusha, Mtwara, Dodoma  na Tanga.

Katika michuano hiyo ambayo imedhaminiwa kwa mamilioni ya fedha na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanajaro Premier Lager, mshindi wa kwanza atazizolea zawadi ya sh. milioni 35, wapili sh.  milioni 20, watatu  milioni tano huku mchezaji bora, kipa bora, mfungaji bora, kocha bora  na timu yenye nidhamu wakipata sh. milioni mbili kila mmoja.

mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages