Breaking News

Your Ad Spot

May 7, 2010

MICHUANO YA KILI TAIFA CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO

*IRINGA KURINDIMA KATIKA UWANJA WA SAMORA
 MICHUANO ya Kili Cup hatua ya makundi inaanza kutimua vumbi leo kwa baadhi ya timu kupepetana katika vituo sita, kikiwemo kituo E cha mkoa wa Iringa.
  Katika kituo cha Iringa, kinachoshirikisha timu za Mapinduzi Stars ya Mbeya, pinda Boys ya Rukwa, Kinondoni  na Ruaha Stars ya Iringa, kipute kitarindima katika Uwanja wa Samora.
  Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Nchini (TFF), katika kituo cha Iringa,  Pinda Boys  na Mapinduzi Stars ndizo zitafungua pazia kwa katika mechi itakayoanza saa 8 mchana, na saa 10 jioni zitashuka dimbani Kinondoni na  wenyeji Ruaha Stars.
Jumapili itakuwa ni mapumziko, wakati timu ya Mapinduzi Stars na Ruaha Stars zikisubiri kushuka dimbani Jumatatu katika mechi itakayoanza saa 8 mchana, na kufuatiwa na mechi ya Kinondoni na Rukwa saa 10 jioni.
  Baada ya mapumziko ya Jumanne, Jumatano zitaashuka dimbani timu za Rukwa na Iringa saa 8 mchana na baadaye Kinondoni na Mbeya nao wataumana saa 10 jioni, mechi ambayo itahitimisha sehemu raundi hiyo ya  makundi ya  michuano ya  Kili Cup kwa kupatikana timu mbili zitakazoingia kimbember cha robo fainali kitakachorindima katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mei 23 na Mei 24, 2010.
 Katika robo fainali hizo, timu nane zitakazofanikiwa kupita hatua ya makundi, zitamenyana kupata nne zitakazoingia nusu fainali ambayo itafanyika Mei 25 na Mei 26, 2010 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Faianali ya michuano hiyo itakuwa Mei 28 na Mei 29, 2010 katika Uwanja.
Vituo vingine ambavyo michuano katika hatua ya makundi itarindima ni Dodoma  ambako zinakutana timu nne katika kundi A,  Kundi B (Tanga), Kundi C (Mwanza), Kundi D (Arusha) na kundi F (Mtwara).
   Msimamizi wa kituo E cha Iringa, Eliudi Mvera alisema jana kwamba timu zote nne wakiwemo wenyeji , na waamuzi wanane wameshawasili tangu juzi katika kituo hicho.
Mvera ambaye pia ni  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF taifa na katibu wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa, aliipongeza TBL kwa maandalizi mazuri ambapo alisema, hadi michuano inakaribia kuifanyika katika kituo chake kila kitu kilichostahili kufanywa na TBL ambao ndi wadhamini wa michuano hiyo kilikuwa kimekamilika.
 Katika michuano hiyo, TBL imetenga kitita cha sh.  Milioni 35 kwa mshindi wa kwanza, wa pili sh. Milioni 20 wakati mshindi wa tatu akipata sh. Milioni 5, huku mchezaji bora, kipa bora, mwamuzi bora, mfungaji bora, kocha bora na timu yenye nidhamu wakiwa wametengewe sh.  Milioni mbili kila mmoja.
Wakati huohuo,  timu za Mbeya, Rukwa na Iringa, jana zilikabidhiwa vifaa vya kushiriki katika michuano hiyo ikiwa ni pamoja na jezi na mipira huku TBL wakitoa pia vifaa kama hivyo kwa marefa katika kituo hicho cha Iringa.

Vifaa hivyo ambavyo ni sehemu ya vile ambavyo TBl ilikabidhi mapema kwa timu zote zinazoshiriki michuano hiyo, vilikabidhiwa kwa viongozi wa timu za Mbeya, Iringa na Rukwa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Iringa.
Akikabidhi vifaa hivyo, Meya wa mji wa Iringa, Amani Mwamwindi alizitaka timu hizo kuonyesha  viwango na mchezo mzuri katika michuano hiyo ili kuonyesha kwamba hatua iliyofanywa na TBL kudhamini ni ya maana na muhimu kwa michezo.

Mwamwindi aliwataka vijana kuitumia fursa ya michuano ya Kili taifa Cup katika kushiriki kikamilifu kuonyesha vipaji vyao katika soka ili kuwa chachu ya baadaye ya mchezo huo.

mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages