Breaking News

Your Ad Spot

May 1, 2010

STARS NA AMAVUBI YA RWANDA

*STARS YASHINDWA KUTUMIA VEMA UWANJA WA NYUMBANI.
* YALAZOMOSHWA SARE YA 1-1

KIKOSI CHATAIFA STARSKIKOSI CHA AMAVUBI
TIMU ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’ imejiweka katika wakati mgumu wa kusonga mbele katika michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) baada ya kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’.
   Matokeo hayo yameifanya Stars kufanya kazi ya ziada katika mchezo wa marudiano utakaochezwa mjini Kigali, Rwanda wiki mbili zijazo.
   Katika mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu zote ziliunza mchezo kwa kasi huku washambuliaji wa pande zote wakihaha kusaka mabao.
   Lakini, kadri muda unavyozidi kwenda, Stars walionekana kupoteana zaidi hasa nafasi ya kiungo na ushambuliaji na kuwapa mwanya viungo wa Amavubi, Baptiste Mugiranza na Haruna Niyonzima kucheza wanavyotaka.
  Jambo hilo liliwafanya mabeki wa Stars, wakiongozwa na Nadir Haroub ’Canavaro’ kuwa kwenye wakati mgumu wa kuwazuia washambuliaji wa Amavubi walionekana kuwa na uchu wa mabao.
  Hata hivyo, Stars ilifanya mashambulizi langoni mwa Amavubi dakika za 14, 20, 25 na 30 kupitia kwa Uhuru Suleiman, Mrisho Ngassa na Jerry Tegete, lakini kutokuwa makini kwa washambuliaji hao kuliinyima Stars mabao.
  Kitendo hicho kiliwapa mwanya Amavubi kucheza wanavyotaka na dakika ya 36, Roger Tchouassi aliipatia timu yake bao baada ya Cannavaro, Kelvin Yondani kuzembea kuondosha mpira eneo lao.
  Goli hilo kuliifanya, Stars kuchachamaa, lakini kutokuwa makini kwa washambuliaji kuliifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa goli hilo.
  Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mabadiliko ambapo Kigi Makasi alitoka na kuingia Mussa Hassan ‘Mgossi’. Mabadiliko hayo yaliipa uhai Stars.
  Stars ilifanya mashambulizi dakika za 48, 55 na 59 kupitia kwa Tegete, Ngassa na Mgossi. Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 61 baada ya Mrisho Ngasa kupachika bao la kusawazisha.
 Shuti hilo la adhabu lililopigwa na Erasto Nyoni, lililotokana na Mgossi kufanyiwa madhambi eneo la hatari na mwamuzi kutoka Sudan, Mohamed Hussein kuamuru lipigwe shuti hilo.
  Baada ya adhabu hiyo kupigwa mpira ulimkuta Ngasa na kuukwamisha wavuni. Bao hilo liliwafanya Stars kuongeza mashambulizi, lakini hadi filimbi ya mwisho, timu zilitoka uwanjani zikiwa nguvu sawa.

MCHEZAJI wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Juma Jabu akijitwisha mpira dhido ya Djamal Mwiseneza wa Amavubi ya Rwanda, timu hizo zilipomenyana jana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa timu zonazoshiriki ligi za ndani (CHAN). Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.   Mrisho Ngasa wa Taifa Stars (kulia) akipambana na Nao Kalisa katika mechi hiyo.MCHEZAJI wa timu ya Taifa ya Rwanda Didie Lapet (kushoto) akipambana na Abdi Kasim wa timu ya Taifa, Taifa Stars, timu hizo zilipomenyana jana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa timu zonazoshiriki ligi za ndani (CHAN).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages