.

MDAU ATHUMANI HAMISI KUREJEA NCHINI MEI 8

Apr 30, 2010

Athumani Hamis
MDAU  muhimu wa siku nyingi katika sekta ya habari, Mpigapicha Mkuu wa gazeti la HABARILEO Athumani Hamis ambaye amekuwa akitibiwa nchini Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka miwili sasa, baada ya kupata ajali ya gari mjini Dar es Salaam, mwaka juzi. atarejea nchini Mei 8, mwaka huu.
  " Aslaam, safari imeiva. Narudi Tanzania Mei 8, saa 12 jioni.
Msisikitike kuniona ktk kiti wheelchair, mikono na miguu haifanyi kazi. Ni kazi ya Mungu, haina makosa". huu ndiyo ujumbe ambao Athumani Hamis ameutuma leo jioni kwa mtayarishaji wa Blog hii. nami nimeona ni vema nanbyo wadau muupate ujumbe huu. 

1 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª